Saturday, 28 April 2012

BAA ZAINGIA UBIA NA MAKAHABA!!!

PAMOJA na juhudi za Serikali kupambana na biashara ya ngono nchini, sasa wanaofanya biashara hiyo wamebuni mbinu mpya kukwepa kuingia mikononi mwa vyombo vya dola. 

Mbinu hiyo mpya ni ya kuendesha biashara ya ngono kupitia kaunta za baadhi ya baa zilizoingia ubia na wanaojiuza kwa mkataba wa kiasi fulani cha fedha inayotokana na biashara hiyo kwa siku. 

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, umebaini kuwa zipo baa kadhaa katika maeneo ya Mbezi Luis, Tegeta, Kinondoni na Sinza, Dar es Salaam zinazoendesha biashara hiyo na baadhi zina vyumba maalumu kwa kazi hiyo. 

Baa hizo zinashirikiana na wanaoendesha biashara hiyo (wanaojiuza) wanaume kwa wanawake, ambapo mteja hupaswa kulipa fedha kaunta ya baa ikiwa amekubaliana naye kwa biashara hiyo. 

Mmoja wa wahudumu wa baa moja (jina tunalo) iliyoko Mbezi Luis, aliliambia gazeti hili kwamba katika baa hiyo, kuna wanawake zaidi ya 13 wanaojiuza na wakishakubaliana na wanaume wanaowanunua, hulipa kaunta na kuendelea na mambo yao hapo hapo au kwingineko kwa mujibu wa kiwango cha fedha alichotoa. 

“Hapa kwetu wanalipia kuanzia Sh 20,000 hadi Sh 150,000, inategemea na aina ya mwanamke, kama anavutia au ni wa kawaida; wakishakubaliana, mnunuzi anakwenda pale (akionesha kaunta) kulipia, hiyo pesa inakatwa kodi ya asilimia 20 ambayo baa inachukua na nyingine anapewa mwanamke,” alidai mhudumu huyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake gazetini. 


 ENDELEA KUSOMA http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=29498

No comments:

Post a Comment