Monday, 30 April 2012

KATIBA IZUIE USHOGA NA UTOAJI MIMBA-MALASUSA!!

WAKATI Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni kuhusu Katiba ikitarajiwa kuanza kazi yake kesho, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa amewataka Watanzania wasikubali kuruhusu mambo yasiyofaa katika jamii kuingia kwenye Katiba kwa kisingizo cha haki za binadamu. 

Malasusa ambaye aliwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu kutoa maoni yatakayosaidia kuundwa Katiba mpya, aliyasema hayo jana wakati wa ibada ya uzinduzi wa jengo la kitega uchumi cha Kanisa la KKKT, Usharika wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam. 

Akihubiri kwenye ibada hiyo iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Malasusa alisema kumekuwa na wimbi la watu wanaotetea mambo yasiyofaa kama vile utoaji mimba na kuruhusu ndoa za jinsia moja kwa kisingizo cha haki za binadamu. 

Alisema katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya KKKT uliofanyika Arusha, moja ya maazimio yaliyofikiwa ni kuhamasisha waumini ambao ni sehemu ya jamii, kushiriki kikamilifu kutoa maoni katika mchakato wa Katiba mpya. 

“Tumeagiza kila mchungaji kuhamasisha wananchi wake kushiriki kikamilifu, tunataka iwe Katiba ya kutuletea maendeleo na kuwa Katiba ya Watanzania na si ya Wakristo au madhehebu au dini ya aina yoyote. 
Tushiriki kikamilifu na kuacha kulalamika baada ya Katiba kukamilika,” alisema. Malasusa alisema ipo haja ya kuangalia madaraka yaliyomo katika Katiba na kuondoa vipengele vyenye kasoro na kuweka vipengele vitakavyoendeleza kudumisha amani


  ENDELEA KUSOMA http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=29542

No comments:

Post a Comment