Tuesday, 1 May 2012

ISHA MASHAUZI: MIMI NA TAARAB TOFAUTI, NI MAISHA TU!!

Msanii wa Taarab nchini, Isha Ramadhan a.k.a Isha Mashauzi amesema kwamba yeye yupo tofauti kabisa na Mziki wa taarab ila anafanya kwa sababu ya kutafuta maisha tu. Alizungumza hayo alipokuwa akiojiwa na mtangazaji wa kipindi cha Mkasi, Salama Jabir.
Isha alisema kwamba mama aliyemzaa mama wa baba yake ni mnyarwanda hivyo walihamia Musoma toka Rwanda ndiyo maana anajiita Mkulya wa kwanza kuimba taarab. 
Alisema alishawahi kuwa MC pia kipindi cha nyuma.Wakati huo alikuwa anafahamika kwa jina la Mama Afrika kwa sababu ya staili yake ya mavazi alokuwa anavaa.
Aisha ambaye ni mama wa mtoto mmoja na liyewahi kuolewa mara mbili na kuachika, alisema ndoa ni nzuri na anaomba Mungu aweze kuolewa tena. Alizungumzia hilo pale salama alipomuuliza labda inawezekana ndoa ya kwanza ilvunjika kwa kuwa alikuwa bado mdogo, Aisha alisema hapana kwani huyo wa pili aliolewa akiwa mkubwa lakini tofauti zao ndiyo ilikuwa sababu ya kuachana. Pia alikana tuhuma ya yeye kuwa na mahusiana na Boss mwenzake Thabit na kusema wapo kikazi tu na si hivyo wanavyozungumza. 
Pia alimalizia kusema kwamba anajua ana thamani kubwa na kila siku inazidi kupanda.

"HONGERA AISHA KWA KUWEZA KUJITAMBUA"

No comments:

Post a Comment