Tuesday 8 May 2012
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU, YADAI KESI YA LULU IKASIKILIZWE MAHAKAMA KUU SABABU NI YA KIUAJI!!!
Akizungumza mahakamani hapo Hakimu mfawidhi AUGUSTINE MMBANDO wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, amesema ELIZABETH anakabiliwa na kosa la mauaji na mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji isipokuwa mahakama Kuu na kuwataka kupeleka ombi hilo katika mahakama hiyo.
Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment