Monday 14 May 2012

WABUNGE MAREKANI WAUNDA KAMATI KUISEMA TANZANIA!!!!

WABUNGE wa Marekani, wanakusudia kuunda kamati ndogo katika Bunge la nchi hiyo itakayotetea na kuisemea Tanzania kwa kila jambo litakalojitokeza katika Bunge hilo. 

Hayo yalielezwa katikati ya wiki hii na Mbunge wa Marekani, Dan Boren alipomtembelea Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mwanaidi Sinare Maajar, jijini hapa. 

Boren, kutoka Oklahoma, alihamasisha na hatimaye kuanzisha kundi la wabunge wenye mapenzi na Tanzania na hatimaye kamati ndogo ya kuisemea Tanzania bungeni humo. 

Mbunge huyo wa chama tawala cha Democrat, ameasisi kundi hilo akishirikiana na wabunge kadhaa wa chama chake na wengine wa Republican, kutokana na kufurahishwa kwao na juhudi za Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuimarisha demokrasia, utawala bora na maendeleo katika sekta za uchumi, nishati, kilimo na mazingira. 

Katika ziara yake kwenye ubalozi huo, Boren akifuatana na Hillary Moffett, Mkurugenzi wa Sheria Bungeni, alimhakikishia Maajar utayari wake wa kuisaidia Tanzania katika juhudi hizo. 
ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=30076

No comments:

Post a Comment