RUKIA ABDALHA ni mtoto wa miaka miwili anayeishi RUANGWA (LUGALO) mkoani LINDI alipata ajali ya kuungua na maji ya moto, ameshawahi kutibiwa katika hospitali ya wilaya RUANGWA ambako alipatiwa huduma ya kwanza na kushauriwa aende katika hospital za NDANDA, NYANGAO au MUHIMBILI. Wazazi wa RUKIA hawana uwezo kifedha na kushindwa kufanya matibabu ya majeraha ya mtoto huyo hadi sasa! Kwa sasa mtoto RUKIA anatibiwa na dawa za kienyeji huko nyumbani kwao, hali ya vidonda sio mzuri inazidi kuwa mbaya siku hadi siku! Vidonda vinazidi kuchimba mwili na kusababisha harufu kali na mateso kwa mtoto huyu. Kwa niaba ya Familia tunaomba msaada wa hali na mali kwa mtoto huyu, tunaomba msaada wa aina yoyote utaoleta mabadiliko kwa mtoto huyu. tuma pesa kwa Victor Richard M-pesa 0755 754494/tigo pesa 0715 754494.
No comments:
Post a Comment