Tuesday, 12 June 2012

MWANA FA AIKANA FREEMASON!!!


MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, amesema kuwa ameshtushwa na habari chafu zinazoenezwa juu yake na kuwataka Watanzania kuacha simulizi za kusadikika na kusimama katika ukweli.
Hayo aliyasema katika mahojiano yake na kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachorushwa na televisheni na Radio East Africa, kufuatia swali aliloulizwa na mtangazaji wake Sam Misago juu ya tetesi kuwa yeye ni muumini wa dini ya Freemason.
“Ifike kipindi Watanzania watambue kuwa si kila mafanikio miongoni mwetu yataletwa na Freemason. Nazushiwa hilo kutokana na aina ya mvuto wangu na kazi zangu, lakini kamwe siwezi kuwa muumini wa dini hiyo,” alisisitiza FA.
Katika kipindi hicho, Mwana FA alitamba kuendelea kubaki juu katika sanaa, kutokana na kufanya mambo kwa umakini, kunakotokana na kuumizwa kichwa kabla ya kutoa singo mpya.
Alitumia fursa hiyo pia kutambulisha na kukitolea ufafanuzi kibao chake kipya cha ‘Ameen’ alichoimba kwa kumshirikisha Dully Sykes.

No comments:

Post a Comment