Aneth Gasto akiwa hospitalini
picha:Mbeya yetu
MAMA wa mtoto, Anneth Gasto anayedaiwa kuchomwa moto na kulazimishwa kula kinyesi na mama yake mdogo na kumsababisha mkono mmoja kukatwa mara baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya , Asera Mkandara tayari amewasili mkoani hapa jana (juzi) usiku.
Akizungumza kwa uchungu huku akitokwa na machozi katika hospitali hiyo mjini Mbeya , mama huyo alisema kuwa hajui nini kimemtokea mtoto wake hadi kufikia kukatwa mkono na kwamba anamshukuru Mungu kwa kumkuta mtoto wake akiwa hai.
“Kwa kweli siju nini kilichomkuta mtoto wangu hadi kufikia kukatwa mkono nilichoelezwa na madkatari ni kuwa, mtoto amekatwa mkono na hali yake inaendelea vizuri,”alisema .
Alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa ndugu zake kwamba anahitajika Mbeya mara moja mtoto amepatwa na matatizo makubwa na kusikia taarifa za mtoto wake huyo kupitia vyombo vya habari.
Mama huyo alisema kuwa huyo ni mtoto wake wa Pili ambapo wa kwanza anaishi na bibi yake na kwamba huyo Anneth alichukuliwa na kaka yake ambaye alimuhitaji kwa lengo la kutaka kumlea.
Alipohojiwa kama baba wa mtoto huyo yupo alijibu kuwa baba wa mtoto huyo waliachana naye mwaka 2008 “ndipo kaka yangu alipo muhitaji mtoto wangu aje aishi naye huku Mbeya.”alisema na kuongeza:
“Nasikia uchungu sana kwa yaliyomkuta mtoto wangu kwani Mungu ndiye anayejua, nawashukuru madaktari kwa kuokoa maisha yake na wale wote waliohusika katika kumuokoa na kumleta mtoto hapa hospitali sina cha kuwalipa Mungu ndiye atakaye walipa”alisema.
Mwanamke anayedaiwa kumfanyia unyama mtoto huyo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya juzi kujibu shtaka linalomkabili, ambapo mshtakiwa alikana shitaka hilo na alirudishwa mahabusu hadi Novemba 22, Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa aliiambia Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Anneth.
chanzo: mwananchi
No comments:
Post a Comment