POLISI jijijini Dar es Salaam inawashikilia wanaume watano wanaotuhumiwa kuwa mashoga kwa tuhuma za kuuza miili yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba, alisema jana kuwa watu hao walikamatwa juzi, majira ya saa 5:00 asubuhi maeneo ya Buguruni Chama wakati askari walipokuwa wakifanya msako.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Sadan Hussein (17), Ranadhan Haji (35), Mathias Machumu (22), Joseph Salum (36), na Jawe Mgaya (35).
Alisema watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa, kwani ni kosa la jinai kufanya vitendo hivyo.
Katika tukio jingine, Kamanda Komba alisema mwanaume mmoja ambaye hajafahamika jina lake amefariki akiwa chini ya mti baada ya kutapikana damu nyingi.
Mwanaume huyo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 45-50 alikutwa juzi majira ya saa 7:00 mchana maeneo ya Vingunguti Majani ya Chai.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, marehemu aliishiwa nguvu ghafla na kupumzika chini ya mti hatimaye kuanza kutapika damu na kufariki muda mfupi baadaye.
Kamanda Komba alisema chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi.
chanzo:daima
No comments:
Post a Comment