Friday 21 December 2012

USHIRIKINA WAHUSISHWA KUZALIWA MTOTO WA AJABU

TUKIO la mwanamke Emeliana  Wilson (17) kujifungua mtoto wa ajabu Desemba 17,mwaka huu katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Songwe mkoani hapa, linahusishwa na imani za kishirikina.Mmoja wa watu waliyomuona mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na macho yaliyoungana, kitu kama pembe katika paji la uso wake na kutokuwa na pua alisema yawezekana kuna mambo ya Kiswahili nyuma ya tukio hilo.
“Huyo mtoto siyo bure, yawezekana mama yake amekwenda kinyume na taratibu anazotakiwa kuzifuata mama mjamzito. Pia huenda kuna watu wabaya wameamua ‘kumchezea’ mama wa watu ili azae mtoto wa ajabu kwa sababu wanazozijua wao,” alidai shuhuda huyo.
Mama wa mtoto huyo akizungumza na mwandishi wa habari wa gazeti moja litokalo kila siku (siyo la Global), alikiri kupata ujazito wa mtoto huyo baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji na kupewa dawa za miti shamba.
Aidha, mama huyo ameomba msaada kutoka kwa wasamaria wema wa kumuwezesha kumlea mwanaye kwa madai kwamba mumewe, Emmanuel Mbukwa ametoweka baada ya kumuona mtoto huyo wa ajabu.
Kwa atakayehitaji kumsaidia mama huyo,  namba 0712707630
chanzo:globalpublishers.

No comments:

Post a Comment