MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Zawadi Jacob anatuhumiwa kumuiba mtoto wa miezi minne Martha Joseph, wilayani Igunga ili kulinda ndoa yake.
Hayo yalibainishwa jana na Kamanda wa Polisi, mkoani Tabora, Antony Lutta, wakati akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake.
Kamanda Lutta alisema tukio la kuibiwa mtoto huyo wa Martina Joseph (21) lilitokea Februari 26 mwaka huu majira ya saa saba mchana katika Mtaa wa Warabuni.
Alisema kabla ya tukio hilo Zawadi alikwenda grosari na kuagiza kinywaji aina ya soda huku akiwa kwenye mawindo ya wizi.
Kwa mujibu wa Kamanda Lutta baada ya Zawadi kuagiza kinywaji hicho, aliomba kumbeba mtoto aliyekuwa na mama yake na kutokomea kusikojulikana hadi alipokamatwa huko Misigiri Singinda akielekea kwa mumewe kwa lengo la kumueleza tayari kishajifungua mtoto wa kike.
Alisema mwanamke huyo anashikiliwa na polisi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili dhidi ya wizi huo wa mtoto.
Akizungumza na Tanzania Daima mama wa mtoto huyo, alisema alipomkosa mwanawe alitoa taarifa polisi.
Alisema taarifa hizo zilipofika polisi, jeshi lilianza kazi yake kwa haraka kuhakikisha mtoto huyo anapatikana, na saa tisa jioni mtoto huyo alipatikana huko Misigiri
chanzo:daima
No comments:
Post a Comment