MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka mkoani Morogoro, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ anatarajiwa kuachia ngoma yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina la ‘Dini Tumeletewa’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Afande Sele alisema katika ngoma hiyo ameshirikiana vema na nyota wa muziki huo, Belle 9.
Alisema ngoma hiyo inazungumzia imani za kidini na matukio yanayoendelea hivi sasa na kuwaasa Watanzania kuachana na mambo hayo na kuishi kindugu kama zamani, ambako pia ameizungumzia hotuba ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Afande alisema ameamua kuachia ngoma hiyo kutokana na migogoro inayoendelea kuibuka nchini juu ya imani za kidini.
“Ujumbe wa wimbo wangu mpya, unahusiana na masuala ya imani za dini, leo hii Watanzania tumefikia hatua ya kutengana kwa dini.
chanzo:daima
“Hii ni hatari, tunapoelekea siko kabisa ndugu zangu, tunatengana, tunapigana, tunaharibiana mali kisa imani ya dini wakati dini zimekuja na tulikuwa na umoja na Watanzania wote ni ndugu,” alisema.
No comments:
Post a Comment