MSANII mahiri wa muziki hapa nchini, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ amesema kuwa albamu yake ya sita inayokwenda kwa jina la ‘Nothing But The Truth’ itasambazwa na Kampuni ya Max Malipo.
Akizungumza katika kipindi chake cha ‘Diary ya Jaydee’ kinachorushwa na runinga ya East Africa (EATV), alisema kuwa kuanzia Mei 31, albamu hiyo itapatikana nchi nzima kupitia Benki ya Posta na popote zinapopatikana huduma za Max Malipo.
Jide alisema kuwa tayari maandalizi ya albamu hiyo kuwafikia Watanzania wote yameshafanyika na kuwataka mashabiki wake kumuunga mkono.
“Nitazindua albamu yangu siku hiyo ya Mei 31, 2013 na itapatikana siku hiyo hiyo katika vituo vyote vya Max Malipo, lakini niwaambie Watanzania kuwa waniunge mkono maana kuna watu wamepanga kuharibu uzinduzi wangu kwa kufanya shoo karibu na eneo ambalo nami nitafanya, lakini mimi niwatake Watanzania waniunge mkono tu,” alisema.
Jide anaachia albamu yake ya sita sambamba na kutimiza miaka 13 tangu aanze kazi ya muziki.
chanzo:daima

No comments:
Post a Comment