Thursday, 13 June 2013

Kwenye ndoa hii nani zaidi (kati ya mke au mume)

Baada ya wanandoa (mke na mume) kuishi maisha ya ugomvi kwa muda mrefu, siku moja mume akampiga sana mkewe, mkewe kakimbilia kituo cha polisi mambo yakawa hivi;

mke; Afande nimepigwa sana nusu kuzirai na mume wangu
Afande; Kwanini akupige kiasi hicho?
Mke;(AKAMSINGIZ­IA MUMEWE) kwa sababu nimejua anauza mdawa ya kulevya
Afande; Mume wako anauza madawa ya kulevya??????
Mke; Ndio afande. nikawa namshauri aachane na biashara hiyo ndio akanipiga
Afande; Twende nyumbani kwenu tukamkamate

walipofika home wakamkuta jamaa kavimba kwa hasira, plisi wakamkwida na kumpa kisago mbele ya mkewe wakimtaka awaoneshe yalipo madawa hayo, mambo yakawa hivi

(MBELE YA MKEWE)
Afande; Tunajua unauza madawa ya kulevya kweli c kweli?
mume; Kweli afande
Afande; Yako wapi hayo madawa?
Mume; Nauza lakini sikai nayo hapa nyumbani
Afande; Yanakaa wapi?
Mume; Yanakaa kwa boss wangu afande
Afande; Boss wako ni nani
Mume; Ni baba mkwe wangu!!!!
MKE WAKE KAZIMIA......


No comments:

Post a Comment