Diamond
Prezzo
MKALI wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na mkali wa hip hop kutoka Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’, wanatarajia kupanda jukwaa moja kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Julai 7 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mratibu wa tamasha hilo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, mpambano huo unatarajiwa kutegua kitendawili cha ‘Nani Mkali’ kati ya wasanii hao kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki na kudai kuwa ana imani itakuwa burudani murua kwa wakazi wa jiji na mikoa ya jirani.
Alisema Diamond ambaye ana tuzo ya Msanii Bora wa Kiume ya KTM, ataoneshana ubavu na mkali Prezzo, ambaye ndiye anayeongoza kwa kupendwa nchini Kenya, hivyo unatarajiwa kuwa mpambano mkali kwa kuwa utakuwa ni kati ya Bongo Fleva na hip hop.
Aliongeza kuwa mpambano huo ambao unahusisha Kenya na Tanzania, kwa upande wa ngumi kutakuwa na Patrick Amonte kutoka Kenya na Thomas Mashali wa Tanzania huku Shadrack Machanje akizichapa na Francis Miyeyusho.
“Ukiachana na ngumi, pia bendi za Msondo Ngoma, Jahazi Modern Taarab na Sikinde zitakuwapo kuhakikisha wanakidhi haja za mashabiki wote watakaojitokeza siku hiyo, huku TMK Halisi na Wanaume Family watawafundisha mashabiki wao staili mpya za uchezaji wao, hivyo hii si ya kukosa,” alisema.
Alivitaja viingilio kuwa ni sh 20,000 kwa VIP, viti vya bluu sh 10,000 na mzunguko sh 5,000. Tiketi zitaanza kuuzwa mapema na vituo husika vitatajwa baadaye.
chanzo:daima
No comments:
Post a Comment