MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewaachia huru watuhumiwa wawili kati ya 11 wa kesi ya wizi wa sh milioni 330 mali ya Jeshi la Polisi baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.
Walioachiwa ni Fortunatus Biseko na Deogratias Lumato. Licha ya kuachiwa kwa watu hao, mahakama imewang’ang’ania watuhumiwa wengine tisa ikiwataka wajitetee baada ya kukutwa na kesi ya kujibu.
Watuhumiwa waliokutwa na kesi ya kujibu ni Vedastus Mafuru, Kennedy Achayo, Adelaida Lwekoramu, Luciana Limbu, Agnes Maro, Mkika Nyasebwa, Edna Amos, Kabisi Hangaya na Joshua Onditi ambao wataanza kujitetea mfululizo kuanzia Juni 24 hadi 28 mwaka huu.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Jenevitus Dudu aliyesema kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi 21 wa jamhuri waliokuwa wakiwakishwa na wakili wa serikali Lasdilaus Komanya na Lugua umewahusa washtakiwa hao.
Ilidaiwa mahakamani hapo kwamba baadhi ya washtakiwa hao walikuwa wafanyakazi wa Benki ya Makabwela ya NMB Meatu, tawi la Mwanhuzi na wengine walikuwa wafanyabiashara.
Katika kesi hiyo namba 40/2010 watuhumiwa hao wanadaiwa kula njama, kughushi na kuiba kiasi hicho cha fedha kwenye akaunti yenye jina la Police -Retention Collection Account No. 2011000015 NMB Meatu.

chanzo:daima
No comments:
Post a Comment