Wednesday, 12 June 2013

Mfanyakazi wa ndani mbaroni kwa kumchinja Pepetua na kumtupa kwenye shimo la taka

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wanane, akiwamo mfanyakazi wa ndani anayetuhumiwa kumuua mfanyakazi mwenzake kwa kumchinja.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana.

Alisema Philemon Laiza (27), mkazi wa Mikocheni B, anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Perptua Maina (30) kwa kumchinja na kisha kutelekeza mwili wake kwenye dampo la takataka.

Kova alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.


Katika tukio la pili, alisema watu wawili; Isaya Mafuru (31) na Yusufu Machela (33), wanatuhumiwa kwa uporaji wa mali za raia wa Sweden, Gisela Bergstorm katika maeneo ya Coco Beach.

Katika tukio la lingine, alisema watu wanne, ambao ni Thenase Benjijimana (26), raia wa Burundi, Said Hassan (37), mkazi wa Mbande, Obadia Bukuku (25) na Benedict Mohamed (32) wakazi wa Tabata, wanatuhumiwa kwa kukutwa na gari ya wizi aina ya Noah T 157 BWC, pamoja na pikipiki aina ya Boxer T 568 CDL.

Wote kwa pamoja wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment