Saturday, 29 June 2013

Utandawazi unapoteza mila za Mtanzania

MAADILI ni utaratibu ambao hutumiwa na watu katika jamii fulani. Kwa Tanzania inaonesha kuwa ni asilimia 49.8 ya watu ndio wanafuata misingi, tamaduni, mila na desturi ya Mtanzania.
Sambamba na hilo, inakadiliwa kuwa ni asilimia 50.2 ya watu wameachana na tamaduni zao za Kitanzania na kuchukua tamaduni za kigeni kutoka sehemu mbalimbali hususani ulaya.
Sababu ya kuiga tamaduni hizo, zipo katika mtazamo tofauti tofauti kwani wapo mwengine kupitia tamaduni hizo za nje kumewasababisha kubadilisha mionekano kwa kuwa mavazi yao.
Vilevile wapo wengine wenye mtazamo wa kwamba maadili ya Mtanzania ni kwa ajili ya mtu asiye jitambua na kuona kwamba maadili ya kigeni ndio sahihi zaidi ya kuwa ndio kwenda na wakati.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mila, Destuli na Maadili katika Kata ya Ihahi iliyopo Wilaya ya Mbarali Mbeya, Frola Mgadagu hiyo inachangiwa na mabadiliko ya kiutandawazi kwani kadri utandawazi unavyozidi kukua, ndivyo maadili ya Mtanzania yanavyozidi kupotea.
Haikuwa kawaida kabisa kwa mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea kufanya biashara ya kuuza mwili, kimsingi inahatarisha afya na malengo ya vijana.
Katika kipindi hiki, vijana wamekuwa si wasikivu kwa walezi na wazazi wao, matokeo yake wengi wao wanajiingiza katika mambo ya kihuni na kusahau kufanya kazi.
Kwa mfano, wengi wanapenda kujifunza mambo kupitia mitandao ya kijamii, ambayo kwa kiasi kikubwa inatumiwa ndivyo sivyo, matokeo yake vijana hujikuta wakijuta kutokana na athari zake.
Mgadagu anasema vijana wamekuwa mbogo hawamjali wala kusikiliza mtu, anatolea mfano kwa kusema utamkuta mtoto wa kike amevaa nguo nyepesi tena yakubana mbele ya wazazi wake hususani mbele ya baba yake kitu ambacho si lengo la maadili ya Mtanzania ukilinganisha na awali enzi za mababu zetu.
Aidha, amezitaja sababu zingine ambazo zimechangia upotevu wa maadili kuwa ni pamoja na watoto wetu wengi kupenda starehe sana kiasi cha kuweka kando maagozo ya Mungu kupitia vitabu vitakatifu.
Kutokana na hali hii ya mabadiliko ya tabia kwa vijana Mgadagu anaiomba serikali na mashirika ya kijamii na wanahabari kufanya juhudi ya kutoa elimu ya maadili kwa jamii kurudisha thamani ya Mtanzaia iliyopotea kwa kipindi kirefu.
Kwa hatua nyingine, anasema ili tuweze kunusuru maisha ya vijana waliopoteza maadili, ni lazima tushirikiane katika kupinga na kutokomeza mila za kigeni hapa nchini ambazo zinazidi kuharibu vijana.
Madhara yanayotokana na kutoweka kwa maadili mengi, miongoni mwake ni kuwepo kwa ndoa za jinsia moja kitu ambacho hatukukitarajia kuwa kinaweza kutokea katika nchi yetu.
Kwa mujibu wa Mgadagu, pia kumekuwepo na mahusiano ya kimapenzi kati ya mzazi na mtoto kitu ambacho ni laana kubwa mbele ya Mwenyenzi Mungu.
Kwa mtazamo wangu hayo yote yanatokana na kutokuwepo kwa elimu bora kwa vijana kuanzia nyumbani, uvivu wa kufanya kazi pamoja na tamaa.

No comments:

Post a Comment