Monday, 7 October 2013

Westgate haijatoa fundisho kwa Dar

Maeneo mengi yenye mikusanyiko mikubwa ya watu jijini Dar es Salaam hayajachukua hatua za usalama kama tahadhari ili kudhibiti uwezekano wa kutokea kwa matukio ya kigaidi . 

 Hofu ya uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Afrika Mashariki inatokana na shambulizi lililofanywa na magaidi wa Al Shabaab katika jengo la biashara la Westgate, jijini Nairobi, Kenya Septemba 14, mwaka huu na kuua watu zaidi ya 65 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 170.

Katika maeneo kadhaa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita zikiwamo hoteli, maeneo ya usafirishaji, taasisi, masoko, maeneo ya biashara na michezo umebaini kuwa ni maeneo machache  yameanza kuchukua tahadhari kwa lengo la kudhibiti matukio kama la Westgate yasitokee.

Hali hiyo imebainika licha ya kauli za viongozi wa vyombo vya usalama kupitia kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, kwamba vimejipanga kukabiliana na matukio hayo na kwamba wananchi wasiwe na wasiwasi.

MAHOTELI

Baadhi ya hoteli za kitalii ulinzi umeimarishwa kwa kuwakagua wageni na watu wanaoingia.

Katika Hoteli ya Serena wageni na watu wote wanaoingia wanakaguliwa katika mashine maalum za utambuzi.Aidha, katika Hoteli ya Hyatt Regency ulinzi umeimarishwa kuanzia nje na kuna walinzi waliovaa nguo zenye nembo ya KK Security.

Kuna taarifa kwamba mameneja wakuu wa hoteli kubwa za jijini Dar es Salaam walikutana wiki iliyopita kujadili namna kujilinda dhidi ya ugaidi katika hoteli zao.
 Habari zinasema kuwa mameneja hao walikutanishwa na ubalozi wa nchi moja ya magharibi.

KARIAKOO

Katika Soko Kuu la Kariakoo, ulinzi umeimarishwa zaidi hasa katika milango mikuu ya kuingilia.

Katika kila mlango walinzi maalum wamewekwa kwa ajili kuangalia usalama na watu mbalimbali wanaoingia na kutoka, na wanapomtilia mtu wasiwasi wanamkagua.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Florence Seiya, alithibitisha kuimarishwa kwa ulinzi kwa kwa ajili ya tahadhari baada ya tukio la Kenya.

Alisema awali walikuwa wanatumia walinzi wao 15, lakini wamelazimika kukodi wengine 45 kutoka katika Kampuni ya ulinzi ya Western Morine ili kuimarisha  ulinzi.
 Pia alisema waliomba msaada kutoka kwa Mkuu wa  Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Msimbazi (OCD) kusaidiana nao na tayari amekwishatoa kikosi maalum kinachoangalia ulinzi katika eneo hilo kwa muda wote.

Aliongeza kuwa zipo baadhi ya ofisi ambazo zimekuwa zikilipiwa bila kufanyiwa biashara ambazo wameamuru zifunguliwe ili kuangalia zimehifadhi nini.
“Hatuwezi kujiamini sana kutokana na haya ambayo yanatokea kwa wenzetu nchi jirani, tumeamua kuimarisha ulinzi kwa kutumia askari wetu wenyewe, wengine tumekodi na pia tumepewa kikosi maalum kutoka kituo cha polisi cha Msimbazi,” alisema Seiya.

CHUO CHA IFM 
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeimarisha ulinzi kwa kuweka utaratibu wa wageni wanaofika kuwa na vitambulisho.
Walinzi katika mageti ya kuingilia chuoni hapo, walisema hatua hiyo imefuatia tukio la Westgate.

 “Sasa hivi wanafunzi wote wanavaa vitambulisho kabla ya kuingia ndani, na mtu ambaye si mwanafunzi anahitajika kutaja jina lake, ofisi anakoelekea na mwenyeji wake anayeenda kuonana naye pamoja na kitambulisho chochote,” alisema mmoja wa walinzi.

Baadhi ya wageni walionekana wakionyesha vitambulisho vya kupiga kura, vya benki na vya kazi. 

Hata hivyo, uchunguzi ulionyesha kuwa ukaguzi wa watu getini ni mdogo kwani licha ya kuwa na vitambulisho, hakuna utaratibu wa kuandikisha majina wageni wala muda walioingia.Aidha, walinzi hawakuonekana kuwa na silaha za kujihami iwapo tukio lolote la dharura litatokea ghafla. 

HOSPITALI YA MUHIMBILI

Katika Hospitali ya Taifa Mhimbili (MNH), hakuna tahadhari za usalama. Walinzi wanaokuwapo kwenye geti kuu la kuingilia kwenye hospitali hiyo, wanawaangalia watu wanaopita na kuingia bila kuwakagua wala kuwauliza vitambulisho.

Kwenye maduka yote ya dawa kwenye hospitali hiyo licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu, hakuna ulinzi wowote, na hata kwenye jengo la wagonjwa wa nje (OPD) idadi ya watu wanaosubiri ni kubwa, lakini hakukuwa  na ulinzi wowote.

Aidha, katika wodi majengo ya wazazi, wagonjwa wa moyo, Chuo cha Sayansi na Tiba, dharura pamoja na wodi za Mwaisela, Kibasila na Sewahaji hakuna  tahadhari za usalama.Aidha katika taasisi ya magonjwa ya mifupa na fahamu (MOI) hakuna tahadhari za usalama.

MLIMANI CITY
Kituo kikubwa cha kibiashara na burudani cha  Mlimani City ambacho kinahudumia maelfu ya wakazi wa Jiji kwa siku, hakijawekewa tahadhari ya ulinzi kutokana na milango mikuu ya kuingilia kutokuwa na ukaguzi kwa watu wanaoingia ndani.

NIPASHE limeshuhudia idadi kubwa ya watu wakiingia bila kukagukiwa licha ya kuwapo kwa askari wanaolinda katika baadhi ya maduka makubwa yaliyomo ndani ya jengo hilo.

Aidha, askari walioko wanalinda katika benki na maduka makubwa. Mbali na kuwapo kwa ulinzi katika maduka hayo, lakini watu wanaoingia katika maduka hayo hawakaguliwi zaidi ya kuzuiliwa wasiingie na vifurushi ama mabegi ndani ya maduka.

Meneja wa Shoprite tawi la Mlimani City, Venance Mathias, anasema baada ya kutokea kwa tukio la Westgate, wameweka milango ya dharura itakayosaidia watu kutoka pindi likitokea tatizo.

“Emergency doors (milango ya dharura) ipo, sisi tumejipanga pindi tatizo litakapotokea tunaweza kuwatoa wateja wetu wote ndani,” anasema Mathias.
 Anaongeza kuwa tatizo kubwa klinalowakabili ni kutokuwapo na sheria inayowaruhusu kumpekua mtu katika mwili.

Meneja msaidizi wa duka la Mr Price, Raphael Katoroki, anasema  katika duka lao wamefunga kamera za CCTV zinazowasaidia kuona baadhi ya matukio.
Alisema ulinzi katika jengo la Mlimani City ni wa asilimia 80 na kwamba baada ya shambulio lla Nairobi, hivi sasa askari wanazunguka zunguka kuhakikisha ulinzi unakuwapo.

Anasema ni vigumu kumgundua mtu aliyebeba bunduki ama silaha yoyote kutokana na kutokuwapo na utaratibu wa ukaguzi wa watu wanapoingia ndani.
Katika eneo la kuingilia magari, kampuni ya ulinzi ya Omega Nitro Risk Solution ndiyo inayofanya kazi ya kuruhusu magari kuingia na kutoka pasipo kuyakagua kama yamebeba vitu hatari.

KIBO COMPLEX

Hali ya usalama katika Kituo cha Kibiashara cha Kibo Complex kilichoko Tegeta Kibaoni jijini Dar es Salaam, ni ya kawaida.

 Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE kwenye kituo hicho kilichokusanya biashara na ofisi za aina mbalimbali kama za maduka ya simu, migahawa, klabu, mabenki, ofisi za TRA na biashara zingine, umeonyesha kuwa  kinatumia walinzi kutoka kwenye kampuni ya binafsi.

Walinzi hao wako kwenye eneo la nje ya jengo, wakifanya kazi ya kuongoza magari na pikipiki zinazoingia na kutoka.

Aidha kuna kibanda cha juu cha mlinzi katika eneo la nje la kuegesha magari kinachotumika kuangalia magari yaliyoegeshwa, na kwa namna kilivyo, kinaweza kutumika kuangalia kinachoendelea katika eneo hilo la nje lililo upande wa kushoto, kuingia sehemu ya mbele ya jengo hilo.

 Kwenye sehemu zote za biashara zilizomo ndani ya kituo hicho zikiwamo benki kadhaa na ofisi, watu wanaingia bila ya kizuizi chochote. Aidha, kituo hicho, hakina kizuizi chochote wakati wa kuingia na kutoka na wakati wa kutoka.

BANDARINI

Kwa upande wa  Bandari ya boti ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar ulinzi ni  mdogo licha ya eneo hilo kuwa na mkusanyiko wa watu.

Baadhi ya wasafiri na wafanyabiashara wa eneo hilo wanasema kuwa hakuna hatua za tahadhari zilizochukuliwa na ili kuwahakikishia usalama abiria.

“Hapa ulinzi haupo zaidi tu ya abiria kukaguliwa anapoingia ndani na   mzingo aliokuwa nao ingawa kuna utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa ajili ya kukatia tiketi ila abiria akiwa hana kitambulisho anatoa chochote pale mlango wa kuingi,” alisema mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe.
Pia alisema, wapo watu wa vikundi shirikishi ingawa    kimaslahi zaidi kuliko kazi.

“Sidhani kama kweli hawa watu wa vikundi shirikishi wanamchango wowote kwa abiria wa eneo hili  endapo kitu chochote cha hatari kitatokea eneo hili,” alisema. 

KITUO MABASI YA MIKOANI UBUNGO
Usalama katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT) siyo ya kuridhisha.

UBT kuna watu wengi wakiwamo wasafiri zaidi ya 12,000 kwa siku na wasindikizikizaji zaidi ya 6,000 wanaoingia na kutoka pamoja na wafanyakazi na wafanyabishara.
Licha ya idadi hiyo kubwa ya watu kuingia katika kituo hicho kila siku, hakuna tahadhari ya ulinzi zaidi ya kuwapo kwa kituo cha polisi ambacho kinajihusisha na kupokea malalamiko ya abiria na wafanyabiashara.

Watu wanaingia na kutoka bila kuwapo ulinzi wala ukaguzi wa aina yeyote zaidi ya kununua tiketi wakati wa kuingia na wakati wa kutoka kukaguliwa tiketi.
Kwa ujumla, kituo hicho hakina ulinzi zaidi ya mlinzi mmoja aliyeonekana akiwa amesimama kwenye geti la kuingilia.

UWANJA WA NDEGE
Licha ya umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), hali ya usalama wake hairidhishi kutokana na magari yanayoingia getini kutofanyiwa ukaguzi zaidi ya kupewa kadi za kulipia ada.Kadi hiyo inapotolewa hakuna upekuzi  ili kubaini gari limechukua kitu gani.

TAZARA
Katika ofisi za makao makuu ya Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) hakuna hatua za tahadhari za usalama kutokana nayo  magari kuingia na kutoka katika eneo hilo bila kukaguliwa.

NIPASHE ilishuhudia ulinzi wa mazoea na siyo wa kuzingatia kwamba matishio ya ugaidi yanaweza kutokea na kuleta madhara.
Eneo linalosimamiwa kwa makini nyakati zote ni ukaguzi wa tiketi na mizigo kabla ya abiria kuingia kwenye treni.

RELI YA KATI

Katika stesheni ya treni jijini Dar es Salaam ulinzi ulioko ni wa kawaida.Walinzi wa kampuni binafsi na polisi wachache ambao wanakuwepo kusindikiza treni ya abiria kupitia kati kwenda Kigoma.

Kimsingi, katika kituo hicho kakuna utaratibu wa kuwakagua wasafiri wanapokuwa wakiingia kwenye treni, hali ambayo inaweza kusababisha wakasafiri wakiwa na vitu vinavyoweza kusababisha milipuko. 

Hata hivyo, Afisa Habari wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mohamed Mapondela, alisema askari wapo kila sehemu, walinzi binafsi na askari Polisi wanaokuwapo treni linapotaka kuondoka na wengine wanasindikiza treni hadi inapofika mwisho wa safari.Alisema tahadhari ipo na kwamba pale tatizo litakapotokea hatua za kiusalama zitachukuliwa, ingawa hakuzitaja.

Wakati hatua za dhati za kuweka tahadhari za kiusalama kukabiliana na uwezekano wa matukui ya ugaidi zikihitajika, Rais jakaya Kikwete katiia hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita, aliagiza watu wote wenye shughuli zenye mikusanyiko kuweka kamera za ulinzi nje nje na ndani pamoja na kuangalia uwezekano wa kuweka vifaa vya upekuzi. vimejipanga kukabiliana na matukio hayo na kwamba wananchi wasiwe na wasiwasi.

MAHOTELI

Baadhi ya hoteli za kitalii ulinzi umeimarishwa kwa kuwakagua wageni na watu wanaoingia.Katika Hoteli ya Serena wageni na watu wote wanaoingia wanakaguliwa katika mashine maalum za utambuzi. Aidha, katika Hoteli ya Hyatt Regency ulinzi umeimarishwa kuanzia nje na kuna walinzi waliovaa nguo zenye nembo ya KK Security.

Kuna taarifa kwamba mameneja wakuu wa hoteli kubwa za jijini Dar es Salaam walikutana wiki iliyopita kujadili namna kujilinda dhidi ya ugaidi katika hoteli zao.Habari zinasema kuwa mameneja hao walikutanishwa na ubalozi wa nchi moja ya magharibi.

KARIAKOO
Katika Soko Kuu la Kariakoo, ulinzi umeimarishwa zaidi hasa katika milango mikuu ya kuingilia.Katika kila mlango walinzi maalum wamewekwa kwa ajili kuangalia usalama na watu mbalimbali wanaoingia na kutoka, na wanapomtilia mtu wasiwasi wanamkagua.

Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Florence Seiya, alithibitisha kuimarishwa kwa ulinzi kwa  ajili ya tahadhari baada ya tukio la Kenya.

Alisema awali walikuwa wanatumia walinzi wao 15, lakini wamelazimika kukodi wengine 45 kutoka katika Kampuni ya ulinzi ya Western Morine ili kuimarisha  ulinzi.

Pia alisema waliomba msaada kutoka kwa Mkuu wa  Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Msimbazi (OCD) kusaidiana nao na tayari amekwishatoa kikosi maalum kinachoangalia ulinzi katika eneo hilo kwa muda wote.Aliongeza kuwa zipo baadhi ya ofisi ambazo zimekuwa zikilipiwa bila kufanyiwa biashara ambazo wameamuru zifunguliwe ili kuangalia zimehifadhi nini.

“Hatuwezi kujiamini sana kutokana na haya ambayo yanatokea kwa wenzetu nchi jirani, tumeamua kuimarisha ulinzi kwa kutumia askari wetu wenyewe, wengine tumekodi na pia tumepewa kikosi maalum kutoka kituo cha polisi cha Msimbazi,” alisema Seiya.

CHUO CHA IFM 
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeimarisha ulinzi kwa kuweka utaratibu wa wageni wanaofika kuwa na vitambulisho. Walinzi katika mageti ya kuingilia chuoni hapo, walisema hatua hiyo imefuatia tukio la Westgate.

 “Sasa hivi wanafunzi wote wanavaa vitambulisho kabla ya kuingia ndani, na mtu ambaye si mwanafunzi anahitajika kutaja jina lake, ofisi anakoelekea na mwenyeji wake anayeenda kuonana naye pamoja na kitambulisho chochote,” alisema mmoja wa walinzi.

Baadhi ya wageni walionekana wakionyesha vitambulisho vya kupiga kura, vya benki na vya kazi. 

Hata hivyo, uchunguzi ulionyesha kuwa ukaguzi wa watu getini ni mdogo kwani licha ya kuwa na vitambulisho, hakuna utaratibu wa kuandikisha majina wageni wala muda walioingia.Aidha, walinzi hawakuonekana kuwa na silaha za kujihami iwapo tukio lolote la dharura litatokea ghafla. 

HOSPITALI YA MUHIMBILI
Katika Hospitali ya Taifa Mhimbili (MNH), hakuna tahadhari za usalama. Walinzi wanaokuwapo kwenye geti kuu la kuingilia kwenye hospitali hiyo, wanawaangalia watu wanaopita na kuingia bila kuwakagua wala kuwauliza vitambulisho.

Kwenye maduka yote ya dawa kwenye hospitali hiyo licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu, hakuna ulinzi wowote, na hata kwenye jengo la wagonjwa wa nje (OPD) idadi ya watu wanaosubiri ni kubwa, lakini hakukuwa  na ulinzi wowote.

Aidha, katika wodi majengo ya wazazi, wagonjwa wa moyo, Chuo cha Sayansi na Tiba, dharura pamoja na wodi za Mwaisela, Kibasila na Sewahaji hakuna  tahadhari za usalama.

Aidha katika taasisi ya magonjwa ya mifupa na fahamu (MOI) hakuna tahadhari za usalama.

MLIMANI CITY 

Kituo kikubwa cha kibiashara na burudani cha  Mlimani City ambacho kinahudumia maelfu ya wakazi wa Jiji kwa siku, hakijawekewa tahadhari ya ulinzi kutokana na milango mikuu ya kuingilia kutokuwa na ukaguzi kwa watu wanaoingia ndani. NIPASHE limeshuhudia idadi kubwa ya watu wakiingia bila kukagukiwa licha ya kuwapo kwa askari wanaolinda katika baadhi ya maduka makubwa yaliyomo ndani ya jengo hilo.

Aidha, askari walioko wanalinda katika benki na maduka makubwa.Mbali na kuwapo kwa ulinzi katika maduka hayo, lakini watu wanaoingia katika maduka hayo hawakaguliwi zaidi ya kuzuiliwa wasiingie na vifurushi ama mabegi ndani ya maduka.

Meneja wa Shoprite tawi la Mlimani City, Venance Mathias, anasema baada ya kutokea kwa tukio la Westgate, wameweka milango ya dharura itakayosaidia watu kutoka pindi likitokea tatizo.

“Emergency doors (milango ya dharura) ipo, sisi tumejipanga pindi tatizo litakapotokea tunaweza kuwatoa wateja wetu wote ndani,” anasema Mathias.
Anaongeza kuwa tatizo kubwa klinalowakabili ni kutokuwapo na sheria inayowaruhusu kumpekua mtu katika mwili.

Meneja msaidizi wa duka la Mr Price, Raphael Katoroki, anasema  katika duka lao wamefunga kamera za CCTV zinazowasaidia kuona baadhi ya matukio.
Alisema ulinzi katika jengo la Mlimani City ni wa asilimia 80 na kwamba baada ya shambulio lla Nairobi, hivi sasa askari wanazunguka zunguka kuhakikisha ulinzi unakuwapo.

Anasema ni vigumu kumgundua mtu aliyebeba bunduki ama silaha yoyote kutokana na kutokuwapo na utaratibu wa ukaguzi wa watu wanapoingia ndani.
Katika eneo la kuingilia magari, kampuni ya ulinzi ya Omega Nitro Risk Solution ndiyo inayofanya kazi ya kuruhusu magari kuingia na kutoka pasipo kuyakagua kama yamebeba vitu hatari.

KIBO COMPLEX
Hali ya usalama katika Kituo cha Kibiashara cha Kibo Complex kilichoko Tegeta Kibaoni jijini Dar es Salaam, ni ya kawaida.

Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE kwenye kituo hicho kilichokusanya biashara na ofisi za aina mbalimbali kama za maduka ya simu, migahawa, klabu, mabenki, ofisi za TRA na biashara zingine, umeonyesha kuwa  kinatumia walinzi kutoka kwenye kampuni ya binafsi.

Walinzi hao wako kwenye eneo la nje ya jengo, wakifanya kazi ya kuongoza magari na pikipiki zinazoingia na kutoka.

Aidha kuna kibanda cha juu cha mlinzi katika eneo la nje la kuegesha magari kinachotumika kuangalia magari yaliyoegeshwa, na kwa namna kilivyo, kinaweza kutumika kuangalia kinachoendelea katika eneo hilo la nje lililo upande wa kushoto, kuingia sehemu ya mbele ya jengo hilo.

Kwenye sehemu zote za biashara zilizomo ndani ya kituo hicho zikiwamo benki kadhaa na ofisi, watu wanaingia bila ya kizuizi chochote.
Aidha, kituo hicho, hakina kizuizi chochote wakati wa kuingia na kutoka na wakati wa kutoka.

BANDARINI

Kwa upande wa  Bandari boti za Dar es Salaam kwenda Zanzibar ulinzi ni  mdogo licha ya eneo hilo kuwa na mkusanyiko wa watu.
Baadhi ya wasafiri na wafanyabiashara wa eneo hilo wanasema kuwa hakuna hatua za tahadhari zilizochukuliwa na ili kuwahakikishia usalama abiria.

“Hapa ulinzi haupo zaidi tu ya abiria kukaguliwa anapoingia ndani na   mzingo aliokuwa nao ingawa kuna utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa ajili ya kukatia tiketi ila abiria akiwa hana kitambulisho anatoa chochote pale mlango wa kuingi,” alisema mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe.Pia alisema, wapo watu wa vikundi shirikishi ingawa  wako  kimaslahi zaidi kuliko kazi.

“Sidhani kama kweli hawa watu wa vikundi shirikishi wanamchango wowote kwa abiria wa eneo hili  endapo kitu chochote cha hatari kitatokea eneo hili,” alisema. 

KITUO CHA MABASI YAMIKOANI UBUNGO

Usalama katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT) siyo ya kuridhisha.

UBT kuna watu wengi wakiwamo wasafiri zaidi ya 12,000 kwa siku na wasindikizikizaji zaidi ya 6,000 wanaoingia na kutoka pamoja na wafanyakazi na wafanyabishara.
Licha ya idadi hiyo kubwa ya watu kuingia katika kituo hicho kila siku, hakuna tahadhari ya ulinzi zaidi ya kuwapo kwa kituo cha polisi ambacho kinajihusisha na kupokea malalamiko ya abiria na wafanyabiashara.

Watu wanaingia na kutoka bila kuwapo ulinzi wala ukaguzi wa aina yeyote zaidi ya kununua tiketi wakati wa kuingia na wakati wa kutoka kukaguliwa tiketi.
Kwa ujumla, kituo hicho hakina ulinzi zaidi ya mlinzi mmoja aliyeonekana akiwa amesimama kwenye geti la kuingilia.

UWANJA WA NDEGE
Licha ya umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), hali ya usalama wake hairidhishi kutokana na magari yanayoingia getini kutofanyiwa ukaguzi zaidi ya kupewa kadi za kulipia ada.

Kadi hiyo inapotolewa hakuna upekuzi  ili kubaini gari limechukua kitu gani.

TAZARA

Katika ofisi za makao makuu ya Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) hakuna hatua za tahadhari za usalama kutokana nayo  magari kuingia na kutoka katika eneo hilo bila kukaguliwa.

NIPASHE ilishuhudia ulinzi wa mazoea na siyo wa kuzingatia kwamba matishio ya ugaidi yanaweza kutokea na kuleta madhara.
Eneo linalosimamiwa kwa makini nyakati zote ni ukaguzi wa tiketi na mizigo kabla ya abiria kuingia kwenye treni.

RELI YA KATI
Katika stesheni ya treni jijini Dar es Salaam ulinzi ulioko ni wa kawaida.
Walinzi wa kampuni binafsi na polisi wachache ambao wanakuwapo kusindikiza treni ya abiria kupitia kati kwenda Kigoma.

Kimsingi, katika kituo hicho kakuna utaratibu wa kuwakagua wasafiri wanapokuwa wakiingia kwenye treni, hali ambayo inaweza kusababisha wakasafiri wakiwa na vitu vinavyoweza kusababisha milipuko. 

Hata hivyo, Afisa Habari wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mohamed Mapondela, alisema askari wapo kila sehemu, walinzi binafsi na askari Polisi wanaokuwapo treni linapotaka kuondoka na wengine wanasindikiza treni hadi inapofika mwisho wa safari.

Alisema tahadhari ipo na kwamba pale tatizo litakapotokea hatua za kiusalama zitachukuliwa, ingawa hakuzitaja.

Wakati hatua za dhati za kuweka tahadhari za kiusalama kukabiliana na uwezekano wa matukii ya ugaidi zikihitajika, Rais Jakaya Kikwete katiia hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita, aliagiza watu wote wenye shughuli zenye mikusanyiko kuweka kamera za ulinzi nje na ndani pamoja na kuangalia uwezekano wa kuweka vifaa vya upekuzi. 
.
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment