Saturday, 2 November 2013

Polisi: Uporaji wa milioni 220 wafanyakazi wanahusika.

Tukio  la uporaji wa Sh. milioni 220, mali ya kampuni ya ujenzi ya Dott, mjini Moshi, limeibua sura mpya baada ya uchunguzi wa awali wa Polisi kubaini kuwa mpango huo ulisukwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Tukio hilo lilitokea juzi baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi kuvamia gari na kumteka Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo, Shuresh Bab (45), na kisha kutokomea na kitita hicho.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa  wamo baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo inayojenga barabara ya Same-Mkumbara kwa kiwango cha lami, ambao wanadaiwa kuhusika katika njama za kuandaa mpango wa uporaji wa fedha za mwajiri wao.
Bab na wafanyakazi wengine,

walikuwa wakisafirisha fedha hizo kwa gari bila ulinzi kutoka benki ya Standard Charted tawi la Moshi kuzipeleka NMB tawi la Mandela.

Juzi asubuhi, majambazi wawili yaliyokuwa yamesimama katika makutano ya barabara ya Arusha na Old Boma mjini Moshi,yalivamia gari lililokuwa na fedha hizo na kumteka Shuresh na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo ambao walimwamuru dereva wake, Wenslaus Mambo asimame na kubadili mwelekeo.

“Baada ya mahojiano ya kina, imebainika kwamba hapakuwa na uporaji, bali ulikuwa ni mpango mahususi uliokuwa umepangwa wa kumwibia mwajiri wao,” alisema Boaz huku akisisitiza kuwa majina yao yatatolewa baadaye.


Wakati uchunguzi huo wa awali wa polisi ukibaini hayo, bado  wakazi wa mji wa Moshi wanahoji zilipo  Sh. milioni 140 kati ya milioni 220 zilizoporwa, licha ya polisi kusema wameokoa Sh. milioni 80.

Haijafahamika ni watu wangapi walioongezeka katika kamatakamata ya polisi, licha ya Kamanda Boaz juzi 
kusema kwamba jeshi hilo lilikuwa linawashikiria watu wanne.

NIPASHE ilipomtafuta, Meneja wa benki ya Standard Charted tawi la Moshi, hakuwa tayari  kutoa ushirikiano wala kujibu
maswali kwamba ni nani kati ya benki hiyo na mteja wao aliyekiuka sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayoelekeza kwamba malipo yoyote yanayozidi Sh. milioni 10 ni lazima yafanyike kwa njia ya uhamishwaji fedha wa kibenki (interbank money transfer).

Badala yake alimtaka mwandishi kuwasiliana na makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam kwa madai 

No comments:

Post a Comment