Wednesday, 19 November 2014

Hadithi ya MWANASHERIA KATILI sehemu ya 6


 Nilirudi haraka na kuketi juu ya sofa.Baada ya dakika 15 nilishuhudia watu zaidi ya hamsini wakitoka ndani ya chumba kile kile alichoingia mchungaji.Wengi wao w...alikuwa wamechafuka damu midomoni na mikononi.Niliogopa sana lakini cha kushangaza hata mtu mmoja hakunisemesha.Walitoka nje na kutokomea pasipojulikana.Haukupita muda mrefu yule mchungaji naye alitoka kama wale wengine,pia alikuwa amechafuka damu nyingi sana.

Sasa endelea.......
Alinipita na kuingia chumba kingine.Baada ya dakika mbili alirejea sitroom akiwa msafi kabisa na kabadilisha zile nguo alizokuwa amevaa. “Mr.Cheo sikiliza kwa makini,kwa chochote ambacho umekiona hapa usithubutu kumweleza mtu yeyote.Endapo utakiuka ninayokwambia maisha yako yatakuwa hatari.”Yule mchungaji alinionya kwa vitisho.Nilitikia kwa ishara ya kuinua kichwa.
“Ok.twende nikakuoneshe mzigo wenyewe.”Alinichukuwa tukaingia chumba kingine.Huko tuliwakuta vijana wengine wakipanga panga mabox.
“Keti hapo”mchungaji alinielekeza sehemu pa kukaa.Baada ya kukaa ndipo aliponionesha mzigo nitakaosafiri nao.
“Hebu fungua hayo mabox aone”mchungaji alitoa agizo na mara moja mabox yalifunguliwa haraka haraka.
Baada ya kutupia jicho niliona unga umefungwa kwenye paketi za mifuko ya nailoni. “Kwani hiyo ni nini?”nilijikuta nikiuliza hilo swali lakini tayari nilishaanza kuhisi ni dawa za kulevya.
“Haya ni madawa ya kulevya aina ya Kokeini.Ukifanikiwa kufikisa Dar-es-Salaam nitakulipa sh.milioni 50.Hapa nitakupa milioni 25 kama advance au we unasemaje?”
“Hapana mchungaji mimi sitaweza kufanya kabisa bishara haramu”wale vijana kusikia hivyo walitoa bastola zao na kunielekezea mimi.
Nilitetemeka sana nikaona huu ndio mwisho wa maisha yangu.Nilihisi wale vijana pia ni Watanzania kwasababu sisi tulikuwa tunazungumza kwa Kiswahili na wenyewe walielewa nilipokataa kupokea yale madawa.
“No!mwacheni aende,Mr.Cheo umekataa kufanya biashara na mimi!isitoshe umezijua siri zangu nyingi wala hutofika mbali hutakuja kujuta,kufa hufi ila cha moto utakiona”Yule mchungaji alifoka kwa hasira na kunitishia kuniharibia maisha yangu.
Niliondoka pale nikiwa na wasiwasi mkubwa moyoni.Kesho yake niliamua kusafiri na kurejea nyumbani.Ile mizigo yangu niliiacha kwa muuzaji wangu nikamwambia anitumie baada ya siku mbili zijazo.Nilifanya hivyo ili kusalimisha maisha yangu katika nchi ya amani Tanzania.Niliamini kuwa endapo nitafanikiwa kufika nchini salama basi hakuna chochote kibaya kitakachonidhuru.
Baada ya siku mbili mzigo wangu uliwasili nchini na polisi walipoukagua wakagundua kuwa kulikuwa na madawa ya kulevya ndani yake.Nilishindwa kuelewa ni nani ameweka madawa hayo kwenye mzigo wangu.Ndipo siku ile nilipokamatwa na polisi mpaka sasa nipo hapa.Moja kwa moja nina wasiwasi na yule mchungaji ndio kanifanyia mchezo huu.”Mr.Cheo alimaliza kumsimulia mkewe kisa kizima na machozi yaanza kumtoka.
“Pole sana mume wangu kwa yaliyokusibu,kumbe ndio hivyo!nimeshagundua kitu!Kwani huyo mchungaji ni yupi?”
“Ok.tafadhali mama muda wa mazungumzo umekwisha.Afande mrudishe huyo ndani.”kabla mke wa Uncle hajajibiwa swali lake,afande wa zamu alimwambia kuwa muda umekwisha hivyo yampasa kuondoka.Mr.Cheo alichukuliwa na kurudishwa ndani,mkewe alihuzunika sana.Aliwashukuru na kuwaaga wale maaskari kisha akarudi nyumbani.
Alipofika kwao alioga na kupumzika.Jioni alimsimulia Mike na dada yake mambo yote aliyoambiwa na mumewe. “Huyo mchungaji anaitwa nani?”Mike alihoji kwa hasira sana.
“Hakuniambia kwa kuwa muda ulikuwa umekwisha na mimi nilitakiwa kuondoka.”
“Nakuhakikishia Aunt lazima nilipize kisasi kwani aliyofanyiwa Uncle yamesababisha hadi mimi kuacha shule.”
“Usiseme hivyo mwanangu ,wewe bado ni mdogo sana hutaweza kushindana na wenye fedha,huoni sisi tumejaribu mpaka tumefilisika.”Mke wa Uncle alimsihi Mike na kumwambia kuwa hayo ni mambo ya dunia tu.Siku ziliendelea kusonga bila Mike kuwepo shuleni.Hatimaye miezi sita ilipita,kila mwisho wa mwezi Mike na Aunt walikwenda kumtembelea Uncle gerezani.
Siku moja Mike akiwa sitroom mara akasikia.. “Hodi!hodi!”
“Karibu!”Mike aliitikia na kwenda kufungua mlango.
“Oooh!Principal karibu sana”Mike alitaharuki na kumsalimia mama mmoja wa makamo.Baada ya salamu Mike alimkaribisha mama yule ndani. “Aunt njoo umuone mwalimu wangu.”Mike alimwita Aunt kisha akamtambulisha kwa mwalimu wake.
“Asante kwa kukufahamu mama,mimi nilikuwa namjua tu Mr.Cheo.Natumaini kuwa wewe ndiye mke wake?”
“Ndio,upo sawa kabisa”Aunt alijibu kwa kujiamini.
“Kwani yeye yupo wapi au amesafiri?”badala ya kujibu Aunt aliinama kidogo huku machozi yakimlengalenga.Mwalimu alipata hofu moyoni.
“Kuna tatizo gani mbona hivyo mama?eti Mike kuna nini?”ilimbidi mwalimu adadisi zaidi.
“Madam kuna matatizo makubwa sana hapa nyumbani ambayo yamesababisha hata mimi kutokuwepo shuleni mpaka muda huu.”Mike alimjibu mwalimu wake huku akimbembeleza Aunt yake aliyekuwa akilia.Baada ya muda kidogo Aunt alinyamaza na kuendelea na mazungumzo.

“Mimi nimekuja hapa kujua tatizo kubwa lililomfanya Mike kutofika shuleni,au umehama?”
“Hapana madam,mimi nipo tu nyumbani tangu January”Ilimbidi Aunt amweleze mwalimu mambo yote yaliyomsibu mumewe.
“Ndio hivyo mwalimu,tuliuza hadi vitu vya ndani mpaka tukafilisika kabisa.Kwahiyo tumekosa ada ya shule ndiyo maana Mike yupo nyumbani”
“Poleni sana kwa matatizo,kama mngesema mpema tungejua tutamsaidije Mike.Ila hamna shida,mimi nitajaribu kuongea na mwenye shule kuhusu tatizo hili kwani hata yeye mwenyewe kahuzunika sana Mike kutokuwepo shuleni.Tulifikiri labda huenda kahama shule kumbe sivyo.Mike ni kijana mzuri sana,mwenye heshima na bidii mno katika masomo yake.Hakuna asiyezijua sifa zake,hakuna tatizo nitawapigia simu kuwajulisha.”
Madam aliwapa pole familia ya Mr.Cheo kisha akaaga na kuondoka zake.Mike alimsindikiza mpaka karibu na gari lake.Baada ya Madam kuondoka Mike alirejea ndani akiwa mwenye furaha baada ya kusikia kuwa kuna uwezekano wa yeye kurudi shuleni.
“Aunt simu yako inaita”Mike alimwita Aunt yake kumjulisha kuwa simu yake inaita. “Helloo!nani?aaah!mwalimu,habari za toka juzi?”Mike alitega sikio kwa makini baada ya kumsikia Aunt yake akiongea na mwalimu wake.
“Mike!Mike!ama kweli Mungu mkubwa.Mwalimu kasema mwenye shule kakubali urudi shule ukamalizie hii miezi sita iliyobaki ili uweze kufanya mtihani wa taifa wa form two”Aunt alimweleza Mike baada ya kukata simu
‘KweliAunt!?Mike alirukaruka kwa furaha tele.
“Yaani Jumatatu hii ijayo lazima uwe umeripoti shule.”Aunt alimkumbatia Mike huku wakicheka mpaka wakaanguka juu ya sofa lililokuwa jirani yao.
“Mike!Mike!”Mike alisikia sauti ya msichana ikimwita chumbani kwake.Alitaka kuitika lakini moyo ukasita.Alifikiri Aunt yake kasikia kumbe sivyo.
Alinyanyuka na kwenda chumbani kwake kisha akafunga mlango kwa ndani.
“Mungu wangu!Caren habari za siku nyingi?kwanza umefikaje kwetu isitoshe mpaka chumbani kwangu?”Mike alitaharuki mara baada ya kumwona Caren mle chumbani.Alipata mfadhaiko wa kimawazo kichwanii kwake.
“Huyu msichana amepajuaje hapa?sijawahi kumwona tangu tulipoonana Kunduchi beach.Wala sikumwelekeza kwetu,sasa amepajuaje?mbona ananipa wasiwasi namna hii?au huyu naye ni jini wa baharini nilikumbana nae?”Mike alijiuliza maswali mfululizo lakini hakuweza kufahamu Caren amefikaje kwao?
“Usiwe na wasiwasi Mike mimi nitakupa mambo yote mazuri unayohitaji kama utakuwa mvumilivu”
“We Caren mbona unanishangaza?”Mike aliendelea kupagawa baada ya kumsikia Caren akimweleza mambo kama yale.Alipomsogelea na kutaka kumshika mara ghafla akabadilika na kuwa na sura nyingine kabisa kisha akaanza kucheka. “Ha!ha!ha!ha!ha!!!”
“Haaaaa!!!kumbe Bahari!mbona unanifanyia hivi lakini?”Mike alishusha pumzi nzito baada ya kugundua kuwa kumbe ni jini Bahari aliyeamua kumfanyia vituko.
“Wala sio hivyo Mike nilitaka tu kukuonesha uwezo wangu.Ninaweza kuvaa sura ya mwadamu yeyote na kufanana naye”
“Kwahiyo unaweza hata kuvaa sura yangu?”Mike alihoji…
“Ndiyo naweza!!Kwanza achana na hayo,Jumatatu unarejea shule kama kwaida.Mimi ndio nimefanya yote haya.Nilikuahidi kuwa nitakusaidia matatizo yako yote.Caren sasa hivi anasoma St.Mary’s tangu January,sikutaka tu kukwambia kwasababu zangu binafsi”.Jini Bahari alimweleza Mike mambo mengi sana kisha akatoweka.
Furaha ya Mike iliongezeka mara dufu baada ya kusikia kuwa Caren anasoma St.Mary’s.Alitamani siku ziyoyome haraka haraka ili Jumatatu iwahi kufika akamwone Caren.Siku zilikatika hatimaye Jumatatu ikawadia.Mike alidamka asubuhi na mapema na kujiandaa kwa safari ya shule.Alichanganya miguu mpaka kituoni kusubiria shool bus.
“Aaah!Mike ulipotelea wapi?mbona ulikuwa huji shuleni?”Wanafunzi walimshangaa sana Mike baanda ya kupanda basi la shule.Wakiwa ndani ya basi Mike alipiga story nyingi sana na wanafunzi wenzake mpaka walipofika shuleni.Baada ya kushuka kwenye basi karibu kila mwanafunzi alimkumbatia Mike na kumuuliza kulikoni mbona kipindi chote hicho hakuwepo shuleni?Mikie aliwaeleza wanafunzi wenzake pamoja na waalimu watatizo yaliyompata Uncle na kusababisha akose mtu wa kumlipia ada ya shule.
“Pole sana Mike,muombe Mungu atakusaidia.”Waalimu pamoja nawanafunzi walimpa pole nyingi mno Mike na kumsihi amtegemee Mungu katika kili jambo.
“Principal yupo wapi”Mike alimuulizia mkuu wa shule.Alielekezwa kisha akaingia ofisini kwake na kumshukuru sana kwa msaada wake uliomwezea kurudi tena shule.
“Haina haja ya kunishukuru mimi Mike,Mungu ndiye muweza wa kila kitu hapa chini ya jua.Yeye ndiye anastaili shukrani hizi mimi ni kama njia yake ya kuleta msaada kwa kondoo wake.”
“Hamna tatizo Madam hilo tayari nimeshalitekeleza muda mrefu.mmmh!Madam naona una ofisi mpya,una maendeleo kweli kweli!”Mike alimtania mwalimu wake.
“Sasa Mike itakubidi usome kwa bidii mno kwasababu vipindi vingi vimekupita ulipokuwa nyumbani,si unajua una mtihani wa taifa?”
“Ndio Madam nitajitahidi kadri niwezavyo,sitakuangusha Madam.”Mike alimwahidi Principal wake kuwa atafanya vizuri.Baada ya mazungumzo mafupi Mike aliondoka kuelekea paredi kwani kengele ilishagongwa kitambo kidogo.
“Jamani Mike!Mike!!Mikeeeeeeeeee!!!!!!!”wanafunzi wote walicharuka kwa vifijo na vigelegele baada ya kumwona Mike.
“Kuna nini tena huko Paredi mbona kelele hivyo?”Caren alimuuliza mwenzake wakiwa wanashuka kwenye basi.Gari lao lilichelewa kufika kutokana na ajali iliyotokea maeneo ya Makonde na kusababisha foleni ndefu mno.Caren alikimbia haraka pared.

**************************
Je nini kitaendelea Caren atakapofika pared na kukutana macho kwa macho na Mike,kijana aliyetokea kumpenda sana tangu siku ya kwanza alipomuona?Usikose sehemu ijayo ya hadithi hii yenye visa na mikasa ya kusisimua.....

**************************
MTUNZI-FREDY MZIRAY

No comments:

Post a Comment