Tuesday, 18 November 2014

Kwanini mke au mume amwibie mwenzake mfukoni akiwa amelala?Baada ya kugundua anaibiwa kiaina na mkewe, huwa analala usingizi wa mang’amumang’amu (wasiwasi) ili amnase lakini wapi. Mwishoni akaona upuuzi akawa anajilalia fofofo. Nikawauliza labda hawatoi matumizi ya kutosha nyumbani wakajibu siyo hivyo, labda ni tabia tu ya wake zao.

Naam. Sikia kituko kingine. Wakati natengeneza nywele katika saluni moja, nikanasa mazungumzo toka kwa kijana mmoja akieleza kisanga kilichotokea usiku wa kuamkia siku hiyo katika nyumba aliyopanga. 

Nikasikiliza kwa makini hasa baada ya kubaini kinafanana na mazungumzo ya hapo juu niliyosikia ndani ya basi.

Ila maelezo yake ni kwamba badala ya mama kusolomoa fedha mfukoni mwa mumewe, mwanaume ndiye aliyechomoa fedha kwenye pochi ya mkewe.

Maelezo yakawa namna hii;- Ipo familia moja ambayo imefunga ndoa yapata miaka miwili sasa na bado hawajabahatika kupata mtoto. Hata hivyo, wawili hawa wamekuwa wakipurukshana kila kukicha na kesi haziishi kwa wakwe kutokana na vitimbwi wanavyofanyiana.


Hivi majuzi ndiyo zogo likabumburuka pale mke aliporejean kutoka msibani akakuta mumewe kachomoa fedha zake pale alipokuwa amezificha na kwenda kujinafasi nazo kwa kimada.

Msiba ule ulimhusu pia mume huyu lakini alipojua kuwa mkewe lazima alale huko, yeye alirejea nyumbani na kusaka fedha za mkewe kila mahala na alipozikuta akazichukua zote na kuishia kwa kimada wake. 

Mkewe aliporejea ndipo akaangalia fedha zake hajazikuta. Alipomuuliza mumewe akawa anakataa kuzichukua lakini ikawa vigumu kuamini kwani mle ndani hakuna mtu wa tatu.

Bibie kuchunguza akaambiwa na majirani kuwa wala mumewe hakulala nyumbani na pia ni tabia yake hata wakati mwingine akijua mkewe kasafiri humleta kabisa huyo kimada nyumbani hapo bila aibu.

Mpenzi msomaji, ama kwa hakika Maisha Ndivyo Yalivyo. Watu mko wawili ndani ya nyumba au chumba ni chenu wawili lakini bado uaminifu kati yenu hakuna. Swali nijiulizalo ni kwamba ; hivi ni kwanini mke amwibie mumewe au mume amwibie mkewe?

Chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment