Monday, 3 March 2014

Mtoto aliyemwagiwa tindikali aanza kuona

Sheikh  wa Msikiti MKuu wa Bondeni, Mustapha Mohamed Kiago (49) na mwanaye Khalid Mustapha (10) wanasadikiwa kumwagiwa tindikali, wanaendele vema.
Wawili hao, wamelazwa kwenye hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwa matibabu, baada ya kumwagiwa kimiminika hicho, hivyo kujeruhiwa shingoni na usoni.
Akizungumza kwa njia ya simu ya kiganjani na NIPASHE Jumamosi jana, Sheikh Kiago alimshukuru Mungu, kwani afya zao zimeimarika na hali ya mwili `kuchoma-choma’ imepungua.
chanzo:nipashe
"Lakini bado tupo wodini na sasa afya zetu zimezidi kuimarika na hasa mtoto wangu ambaye alikuwa hawezi kufumbua macho kwa jana, ila leo anaweza kuangalia," alisema Kiago.
Alisema kutokana na hali ya mtoto wake kuwa mbaya kwa jana, alilazimika kuhamia wodi ya watoto. 
Juzi, Sheikh huyo  na mwanaye walilazwa hospitalini hapo baada ya kumwagiwa tindikali na mtu asiyefahamika, wakati wakiingia msikitini kuswali.

No comments:

Post a Comment