NYOTA wa mipasho, Isha Mashauzi ameandaa onyesho maalum la utambulisho wa albamu yake mpya iitwayo ‘Nani Kama Mama’, kwenye ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam Juni 23 mwaka huu.
Mratibu wa onyesho hilo, Hamis Mujibu alisema kuwa, utambulisho huo umepangwa kuanza kurindima majira ya saa 3:30 usiku na kuendelea hadi majogoo.
Aidha, Mujibu alisema kuwa, kiingilio katika onyesho hilo la utambulisho wa albamu hiyo ya 'Nani Kama Mama' kitakuwa ni sh 5,000 ambako wasanii kadhaa wanaotamba sasa kwenye mipasho wamealikwa
kutumbuiza.
“Wasanii walioalikwa kutumbuiza kwenye onyesho hilo ni pamoja na Khadija Kopa wa TOT Taarab, Haji Mohammed na Afua Suleiman wa East African Melody,” alisema Mujibu na kuwaomba wapenzi na mashabiki kuhudhuria kwa wingi.
No comments:
Post a Comment