Wednesday, 8 June 2011

MAINDA ANOGEWA KUREMBA WASANII!!!!!!!!



MSANII wa filamu na maigizo, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema ndoto yake ya baadaye ni kufungua duka kubwa la vipodozi litakalofanya shughuli za kuwaremba wasanii wa filamu na maharusi.
Mainda alisema kuwa akili yake kwa sasa haipo katika kumiliki kampuni ya kutengeneza filamu kama ilivyo wenzake aliokuwa nao kwenye fani muda mrefu.
“Kuanzisha kampuni ya filamu si ndoto yangu, nataka kuwa tofauti kwa kuwa na duka la vipodozi kwa sababu tayari nimekuwa nikiwafanyia ‘make up’ wasanii mbalimbali, hivyo naamini tayari natembea na soko mkononi,” alisema.
Kuhusu suala la wasanii wengi kuwa watayarishaji wa filamu na wakati huo huo waigizaji, dada huyu alisema kitendo hicho kwa upande wake anaona kinawanyima watu wengine wenye vipaji kuingia katika fani hiyo.
 “Ukweli ni kwamba kwa sasa wasanii wanaomiliki kampuni za filamu wamekuwa wakifanya kazi na watu wao, yaani hao hao utawakuta katika kila filamu, zaidi kabadilishwa nafasi ya kucheza, kwa kweli hili linawanyima fursa wasanii wanaochipukia, na hivyo kupoteza ladha nzima ya filamu kwani watu wanapenda kuona vionjo tofauti tofauti,” alisema Mainda.


No comments:

Post a Comment