Wednesday, 8 June 2011

CLOLETHA AGEUKIA KAZI YA UPISHI.


MSANII wa maigizo na filamu hapa nchini Coletha Raymond ‘Coletha’, ameanzisha kampuni yake ya kupika vyakula na kupamba katika hafla mbalimbali.
Akiitonya Sayari, alisema kampuni yake hiyo inayoitwa Coletha Catering and Decoration ina uwezo wa kutoa huduma kwa watu wengi kwa wakati mmoja kutokana na kuwa na vitendea kazi vya kutosha.
Akieleza sababu ya kuingia katika kazi hiyo, alisema yeye kama binadamu wengine wenye mahitaji, hawezi kutegemea kazi ya usanii tu katika kuendeleza maisha yake, isipokuwa ni lazima achakarike na upande mwingine.
“Kama mnavyojua kazi za filamu, ipo siku kazi inadoda, sasa ukibaki unaitegemea hiyo tu, inakula kwako, na hii ndio sababu kubwa iliyonifanya nigeukie na upande huu,” alisema.

No comments:

Post a Comment