Monday, 6 June 2011

JACKLINE WOLPER ALIKIMBIA JIJI !!!!!!!!!!!!!!!!!!!



MUIGIZAJI mahiri wa filamu hapa nchini, Jackline Wolper, amelikimbia jiji la Dar es Salaam na kujichimbia mkoani Mbeya ikiwa ni katika harakati za kurekodi filamu mpya inayokwenda kwa jina la ‘God is Great’.
Wolper atashiriki katika filamu hiyo iliyotayarishwa na Kampuni ya Mbeya Film Production ya mjini Mbeya, akiwa na wakali wengine kutoka Bongo.
Mmoja wa wakurugenzi wa Mbeya Film Production, Ombeni Kachota alisema kuwa filamu hiyo ni hadithi ya kweli na imewachukua muda mrefu katika kurekodi, lengo likiwa ni kuhakikisha ujumbe uliokusudiwa unafikiwa kwa kiwango kile kile bila ya kutumia njia ya mkato.
 “Mbeya Film imekusudia kutengeneza filamu zenye ubora mkubwa na kukidhi vigezo vya maadili ya Kitanzania, pia kuhakikisha vijana wa Mbeya wakijiongezea ajira kupitia kazi tunazofanya,” alisema.
Aliongeza kuwa wameamua kuwashirikisha wasanii kutoka Dar es Salaam ikiwa ni katika harakati za kuwaongezea ujuzi wa kisanaa wasanii wa mkoa huo na maeneo jirani ambao watakuwa wakishirikiswa.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa kampuni hiyo kumtumia msanii nguli katika moja ya filamu zake. Awali ilimshirikisha msanii nyota na mahiri katika tasnia ya filamu hapa nchini, Steven Kanumba katika filamu ya ‘Lethal Poison’.




No comments:

Post a Comment