Friday 16 September 2011

AUNT EZEKIEL, JB, RICH, NDANI YA ISIDINGO!!!!!!!!!!!!!!!


                                                                   



KATIKA kuonesha kuwa kazi za wasanii wa filamu nchini zinakubalika hata nje ya nchi, wasanii Jacob Stephen ‘JB’, Single Mtambalike ‘Rich’ na Aunt Ezekiel, wametakiwa kwenda kuigiza katika tamthilia ya Isidingo nchini Afrika Kusini inayorushwa nchini na kituo cha televisheni cha ITV.
Hayo yalibainishwa wiki hii na mmoja wa wajumbe wa Shirikisho la Wasanii, Michael Sangu, wakati wa mahojiano katika kipindi cha TAGz kinachooneshwa katika kituo cha televisheni cha DTV.
Sangu alisema tayari wameshapata barua ya kuombwa kwa wasanii hao kutoka katika kampuni inayotengeza tamthilia hiyo iliyopo Afrika Kusini, na sasa wako katika hatua za kuwakutanisha ili waweze kuingia mikataba.
Aidha, mjumbe huyo aliongeza kuwa, hata waliotengeza filamu ya Neria nao wameshaonesha nia hiyo ya kuwataka wasanii hao wanaotamba katika tasnia ya filamu nchini.

No comments:

Post a Comment