Friday 16 September 2011

HEMED NA MLELA KUMALIZA BIFU.....KUAMUA KUCHEZA FILAMU "RED MZULA"



KATIKA kuonesha kuwa, Watanzania wanapenda amani, wadau wa filamu nchini wamefurahishwa na taarifa kwamba wasanii wawili wanaotesa katika anga za filamu, Yusuph Mlela na Hemed Suleiman wamemaliza bifu lao la muda mrefu na kuamua kucheza tena filamu moja inayoitwa ‘Red Mzula’ inayotarajiwa kuingia sokoni muda wowote kuanzia sasa., baadhi ya mashabiki hao, walisema hii ndiyo desturi ya Watanzania na si kama vijana hao walivyokuwa awali wakirushiana madongo katika vyombo vya habari, na hata kufikia hatua ya kuzichapa kutokana na sababu ambazo hazikufahamika, huku kila mmoja akijiona yuko juu zaidi ya mwenzie.
“Kwa kweli tunasubiri hiyo filamu kwa hamu ili tujionee wawili hawa jinsi ambavyo wamejiachia, kwani bifu si ishu na isitoshe inawashushia thamani waliyo nayo wasanii hao, napongeza sana hatua waliyofikia ili kuweza kuendeleza tasnia hii ya filamu,” 

No comments:

Post a Comment