Friday 17 February 2012

DAVINA AANZA MWAKA VIZURI


MWANADADA Halima Yahaya, aliye maarufu kwa jina la kisanii la Davina, mwaka huu huenda akafuata nyayo za Jacqueline Wolper baaada ya kuanza kushirikishwa katika filamu nyingi, 
Davina aliyezaa na muongozaji nguli wa filamu  William Mtitu, alipotea katika tasnia ya uigizaji baada ya kuingia kwa kishindo, akipaishwa na Kundi la Kaole.
Mpaka sasa Davina ameshatajwa kushiriki katika filamu ya Steve Nyerere itakayoitwa ‘Respect Nyerere’ na filamu ya Rich itakayokwenda kwa jina la ‘Diana’ ambazo zote zinatarajia kuachiwa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment