Friday 17 February 2012

KANUMBA ANA MAPANGO WA KUGOMBEA UBUNGE?


MWIGIZAJI anayetingisha kwenye tasnia ya filamu nchini, Steven Kanumba, amesema hana mpango, wala hawazii kutaka kuwania ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini.
Kanumba aliyasema hayo baada ya kuwepo kwa tetesi kwamba ana mpango wa kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Katika mahojiano na Sayari, Kanumba alisema haoni haja ya kujiingiza katika siasa kwa kuwa kwake haioni kama ina maana sana.
“Sioni kama siasa ina maana kwangu, wengi waliokuwamo humo (kwenye siasa), nilitegemea wangeweza kuwatetea wasanii wa filamu, lakini ndio kwanza wamekuwa wakiwakandamiza kutokana na sheria mbalimbali ambazo wamekuwa wakiwawekea.

No comments:

Post a Comment