Friday, 23 March 2012

JINI KABULA AZUNGUMZIA JUU YA SWALA LAKE LA KUTAKA KUOKOKA!!!!


Kwa kweli nashukuru maombi ya wazazi wangu yameitikiwa, na ninajuta kwa yale ambayo nilikuwa nikiyafanya, nadhani ni shetani tu aliniteka. Nataka mashabiki wangu wafahamu kwamba Kabula wa sasa si yule wa zamani, japokuwa kuokoka kwangu hakutanizuia kuonekana katika filamu mbalimbali kwani mimi bado nitabaki kuwa msanii,” anasema.
Akizungumzia uamuzi wake wa kuokoka wakati alikuwa ni kati ya wasichana waliokuwa wakipamba magazeti ya udaku kila kukicha kwa habari mbaya, Jini Kabula anasema ulokole upo katika familia yao na siku zote wakati alipokuwa akifanya mambo ambayo yalikuwa hayampendezi Mungu, wazazi wake walikuwa wakimuombea usiku na mchana aweze kubadilika.
Kabula anasema kwamba si yote yaliyokuwa yakiandikwa juu yake yalikuwa ya kweli, lakini kwa kuwa alikuwa mtu maarufu, magazeti nayo yakawa yanatumia jina lake ili yaweze kuuza.
Katika wito wake kwa wasanii wenzake dada huyu anasema ni vyema wakamtegemea sana Mungu katika kufanya kazi zao, kwa madai kwamba wasanii wengi kwa sasa wamekuwa wakitumia ushirikina jambo ambalo si zuri.
JINI Kabula ni jina linalotingisha katika fani ya uigizaji.
Dada huyu ambaye jina lake la kuzaliwa ni Miriam Jolwa, alianza kujizolea umaarufu kupitia igizo la ‘Jumba la Dhahabu’ lililokuwa likirushwa na kituo cha Star Tv.
Jini Kabula kwa sasa anatesa pia katika tamthilia ya ‘Milosis’ inayooneshwa katika kituo cha TBCI, historia yake inaonesha kwamba alizaliwa wilayani Bunda,Mkoani Mara ambapo elimu yake ya Msingi aliichukulia katika shule ya Makongoro mwaka 1995 hadi 2002 na baada ya hapo alijiunga na shule ya sekondari Mwanza kabla ya kuingia kwenye mambo ya urembo na uigizaji.

No comments:

Post a Comment