WAKATI siku za karibuni msanii Steven Kanumba, akianika wazi kuwa wana ugomvi na msanii mwenzake Vincent Kigosi ‘Ray’, sasa jambo hilo limejidhihirisha wazi.
Habari zinapasha kuwa, Kanumba alishindwa kutokea kwenye sherehe za kuadhimisha kuanzishwa kwa Umoja wa Bongo Movies zilizoratibiwa na Mwenyekiti wa Umoja huo, Jacob Steven ‘JB’ na Ray, na kufanyika katika ukumbi Bussiness Park, maeneo ya Makumbusho, jijini Dar es Salaam, zikiwakutanisha wanasii mbalimbali na wadau wa tasnia ya filamu.
Wadau mbalimbali waliozungumza na Sayari, walisema Kanumba alishindwa kutokea katika sherehe hizo kwa kuwa zilikuwa zimeshikwa kidedea na hasimu wake, Ray, hivyo ingekuwa ngumu kukaa naye eneo moja na hivyo akaona bora azipoteze

No comments:
Post a Comment