Monday, 5 March 2012

KANUMBA: NILIMSHITAKI WEMA KWA BARAKA ZA WAZAZI WAKE!!!!

MWIGIZAJI nguli wa filamu, Steven Kanumba amesema wazazi wa Wema Sepetu walimuunga mkono kwa kitendo chake cha kumshitaki polisi mrembo huyo aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, kutokana na fujo ambazo alimfanyia.
Mastaa hao wawili wa filamu ambao hapo siku za nyuma walikuwa wapenzi, walifikia hatua hiyo baada ya Wema kumvunjia kioo cha gari Kanumba.
Akizungumza katika kipindi cha ‘Mkasi’ kinachorushwa na kituo cha televisheni cha East Africa - EATV, Kanumba alisema kabla ya kufanya maamuzi hayo, aliwasiliana na wazazi wa Wema ambao nao kwa kuwa walishachoka na tabia zake, walimpa ruhusa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment