Monday, 12 March 2012

USHIRIKINA WAWATIA HOFU WANAKIJIJI!!

WAKAZI wa kijiji cha Kisanga, kata ya Kisanga, tarafa ya Mikumi, wilayani Kilosa, Morogoro, wameingiwa na hofu, wakihisi ndugu zao wamekufa kutokana na njia ya kishirikina. 
Hofu hiyo ilikuja takriban wiki tatu zilizopita baada ya Padre wa shirika la Stigmatine, Harisson Mulenga, ambaye ni paroko wa parokia ya Kisanga, kwa kushirikiana na watumishi wengine wa kikundi cha maombi cha Karismatiki kuendesha maombi katika kijiji hicho, ambapo wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Kisanga walianguka huku wakikiri kuwa ni washirikina na wameshiriki katika mauaji ya watu kadhaa.
Katika mahojiana  na wanafunzi hao, Teresia Deo, Perpetua Ananias, Jenifer Masheri na Happiness Mtindi, Tanzania Daima, lilisimuliwa jinsi walivyokuwa wakifanya ushirikina huo kwa kuhusika katika matukio tofauti ya mauaji.
Hali hiyo ilileta hofu kubwa kwa walimu wa shule hiyo, hatua iliyomfanya mmoja wao, Mwalimu Joseph, kuomba uhamisho. 
Hata hivyo, watoto hao walisema kuwa hawajapenda kufanya mambo ya kishirikina bali kuna watu wakubwa ambao wamekuwa wakiwatumia.
Waliwataja watu hao kuwa ni Melania Kusira, Antonia Kibua, Simon Kusira, Pesambili, Lucy Mkalawa, Paulina Shemuhunge, Cosmas Kusira na Eveta Mpamba (Mama Gire).
Madai hayo yaliufanya uongozi wa kijiji kuwaita watuhumiwa hao mbele ya watoto hao ili kuthibitisha tuhuma hizo, lakini walikataa kuhusika.
Baada ya tatizo hilo kushindikana kutatuliwa katika ngazi ya kijiji, walimu nao ikawabidi wamuite ofisa elimu wilaya ili kumwambia matatizo ambayo yanawapata kiasi cha kukosa hamu ya kufundisha.
Baadhi ya wananchi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walielezwa kusikitishwa na vitendo hivyo kwani hata baadhi ya viongozi wa dini walitajwa na watoto hao kuwa wanajihusisha na ushirikina.
Mpaka sasa tatizo hilo lipo katika ofisi ya mbunge wa Mikumi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilosa, Mohamed Magi, huku kamati ya ulinzi na usalama ikifanyia kazi.
Naye, Paroko Mulenga, amewasimamisha kazi watu wawili, Melania Kisura (Mama Cathy) na Simon Kisura, waliokuwa wakifanya kazi parokiani kwa sababu ya tuhuma hizo

No comments:

Post a Comment