MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imebaini zaidi ya polisi 700 na wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 248 wakiwa wameghushi vyeti vya shule.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu alisema jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu za kuchelewa kutoa vitambulisho vya Taifa vilivyotarajiwa kuanza kutolewa mwanzoni mwa mwezi huu.
Kutokana na udanganyifu huo, Maimu alipendekeza kiundwe chombo maalumu cha kuchunguza hali hiyo.
“Katika uzoefu tuliopata katika majaribio ya utoaji vitambulisho, tumebaini baadhi ya waombaji ambao wameonekana kutumia vyeti visivyo vyao, hivyo tumeona kuwapo haja ya kuwa na chombo maalumu cha uchunguzi, ili kujihakikishia kunakuwa na taarifa sahihi,” alisema Maimu.
Kuhusu kuchelewa kutoa vitambulisho hivyo, alisema kulitokana na mabadiliko makubwa katika mfumo wa daftari la kielektroni la anuani za makazi na simbo za posta na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=30154
No comments:
Post a Comment