Tuesday 5 June 2012

MTOTO WA KIGOGO AFANYA PATI YA BUNDUKI!!!

MTOTO wa kigogo serikalini, Peter Rupia amefanya pati ya bunduki.
Peter alifanya pati hiyo hivi karibuni nyumbani kwake, Mbezi Beach, Dar es Salaam akiwashirikisha marafiki zake ambapo walilewa na kulengana shabaha wakati risasi zikiwa ndani ya bunduki.
Huku akitambua kuwa ni kosa kisheria, Peter aliruhusu silaha hiyo ya moto itumike kuwatishia wanawake (kwa utani) ambao walikuwa wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kusalimu amri.
Uwazi lina picha zinazoonesha jinsi pati hiyo ya bunduki ilivyofanyika ambapo baadaye wahusika walipolewa chakari, walivua nguo na kufanya vitendo visivyoandikika gazetini. 
Shuhuda wa tukio hilo, alisema bunduki hiyo aina ya ‘shortgun’ kwanza alipewa kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Sammy lakini baadaye kila aliyekuwa na hamu ya kuichezea, hakukuwa na kipingamizi cha kufanya hivyo.
Hata hivyo, aliyetia fora kucheza na silaha hiyo ni Sammy ambaye alikuwa akiichukua bunduki hiyo na kulenga mbingu au muelekeo wa bahari huku wasichana waliokuwa wamelewa wakifurahia kitendo hicho bila kujua hatari ya kuchezea chombo hicho kilichokuwa na risasi za moto sita.
Habari zinasema kuwa Sammy licha ya kulenga bunduki huku na kule, alikuwa akiichukua bunduki hiyo na kuzunguka nayo kwa wasichana mbalimbali ambao nao walikuwa wakiigusa huku akiwa ameikumbatia mfano wa mtoto mchanga, akiwa amevaa bukta na kubaki kifua wazi.
“Sisi tulishangaa, kwa nini sehemu ya ulevi kama ile itolewe bunduki ndani tena ikiwa na risasi na kupewa watu kuichezea? Huko ni sawa na kumchezea sharubu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema,” alisema mtoa habari wetu.
Habari zinasema awali ilikuwa haijulikani bunduki hiyo ilikuwa ya nani lakini baadaye wakagundua ni ya Peter kwani alionekana kuibeba na kuiweka ndani.
ENDELEA KUSOMA  HAPA:http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/mtoto-wa-kigogo-afanya-pati-ya-bunduki

No comments:

Post a Comment