Wednesday, 6 June 2012

MWANAHABARI ATHUMAN HAMISI AONGELEA MUAASTAKBALI WA MAISHA YAKE (MICHUZI B...


 Ukweli kwa sasa Account ya CRDB ilikuwa maalumu kwa ajili ya kusomeshea watoto, imekauka ya Postal bank ambayo  ya mshahara haina kitu. Pesa ya mshahara inayoingia benki ni 450,000

Nawalipa nurse, msaidizi wake na mfanyakazi 370,000. Maisha ya ulemavu ni ghali sikutarajia . nina wanangu watatu, wa kwanza anamaliza darasa la saba mwaka huu, wa pili yuko la nne na wa mwisho yuko la pili.

Hawa wanasoma primary za kulipia wote hawa nawalipia 200,000 kila mmoja kwa term jumla 400,000 hizo shule zina term nne kwa mwaka. Gharama chakula, vifaa vya wanafunzi, gharama zao ndogondogo na za kifamilia Pamoja na chakula kwa mwezi , inakwenda kati ya 750,000 mpaka 900,000 kwa mwezi.

Nimekuwa ombaomba mpaka watu kadhaa siwalaumu, wamechoka hawapokei simu wala kujibu sms  . siyo siri ndugu wote wamekimbia waliobaki ni marafiki wa kweli wameniingiza katika familia zao. Hali yangu ni mbaya sana kiuchumi.

Sina uwezo wa kulipa nyumba kwa gharama zozote zile. Mimi Athumani Hamisi, naomba watanzania watakaoguswa wanisaidie. Kubwa nyumba na ushauri wa madaktari walinishauri nisiishi mbali na mazingira ya hospitali kulingana na hali yangu.

Makampuni , mashirika, wizara yoyote, shirika la nyumba la Taifa NHC, watu binafsi, serikali na Taasisi yoyote watakaoguswa na kilio changu nawaomba wanisaidie kwa njia yoyote . kwa walio tayari  naomba misaada ipitie katika account No 01J2027048800 ya CRDB na Account No 010-00090488 ya Postal Bank

chanzo:http://josephatlukaza.blogspot.co.uk/

No comments:

Post a Comment