Wednesday 6 June 2012

UBAGUZI UTAKAOISUMBUA SOKA NA EURO 2012!!



Vikosi vya timu nyingi zinazoshiriki Euro 2012 vina mchanganyiko wa watu wenye asili tofauti, jambo ambalo Ulaya ya zama hizi inatakiwa izowee.
Yapo mengi ya kuvutia kuhusu mpira wa miguu barani Ulaya kwa sasa, lakini hili la watu wa asili ya nje ya Ulaya linaonekana kuwatumbua nyongo Wanazi mamboleo na wanaowachukia wahamiaji.
Ni bahati mbaya pia kwamba hili limefufuka kwa kuibukia kwenye siasa za Ulaya na dalili zake zimeanza kubainika kwenye viwanja vya soka barani.
Ama kwa hakika, mashindano ya Euro 2012 yanayokutanisha timu 16 bora za mataifa ya Ulaya nchini Poland na Ukraine kuanzia mwezi huu, sasa ni kumbusho kwamba maadui bado ni sehemu ya soka ya Ulaya.
Katika mashindano haya makubwa yanayoendeshwa kwa mtindo unaokaribia ule wa Fainali za Kombe la Dunia, tayari familia za wachezaji wawili weusi wa England zimevunja ratiba zao

No comments:

Post a Comment