Wednesday 24 October 2012

CHONDE-CHONDE POPOTE ULIPO SAIDI KUBADILISHA MAISHA YA ALLY HABIBU KIEKI!!!











Jina Kamili: Ally Habibu Kieki
Kuzaliwa: 1981
Kabila : Mmatumbi
Hali ya Ndoa : Ana mke na watoto 2


Historia
Tarehe 6 mwezi Januari  mwaka  2009 ni siku ya historia kwa ndugu yetu  Ally Habibu Kieki mkazi wa Mbagala Kipati aliyekuwa  akifanya biashara zake maeneo ya Chanika Msumbiji. Ally  kwa kipindi hicho alikuwa akifanya biashara ya  Malimao, Machungwa na mihogo huko Chanika na kuuza bidhaa zake katika masoko  ya Ilala na Buguruni.

Kama ilivyoada kwa wafanyabiashara wa aina yake siku hiyo Ally aliamka asubuhi na mapema  kwenda kufanya manunuzi yake  ili alete mzigo Sokoni,  akiwa njiani na baiskeli alivamiwa na watu wane waliompiga mapanga hadi kuzirai , Ally alipoteza damu nyingi na mikono yake kuharibika kabisa kiasi cha kukatwa na kubaki kilema hadi leo hii.
Watu hao pamoja na kumfanyia Ally unyama huo pia walifanikiwa kuondoka na baiskeli yake, fedha taslimu  shilling laki 7 na baadhi ya Vitambulisho vyake. Kwa bahati nzuri  wasamaria wema waliweza kutokea eneo la tukio baada  ya masaa kadhaa na kumpeleka Chanika Police kwa ajili ya kutoa taarifa na hatimaye katika hospitali ya Amana Ilala alikopatiwa huduma ya kwanza na kupelekwa Muhimbili alikolazwa kwa muda wa mwezi mmoja.

Kutokana na uwezo mdogo kifedha Ally alishindwa kumudu gharama za Hospitali ya Muhimbili na hivyo kuamua kurudi nyumbani kwa baba yake Mbagala akiwa na mchumba wake aliyedumu nae kwa miezi nane na yeye kuamua kurudi kwa wazazi wake.

Safari ya matibabu ya Ally haikuwa rahisi ilikuwa ni ngumu na mateso mengi kiasi cha ndugu na jamaa kushindwa kumudu na kumuona kama mzigo mkubwa kutokana na ugumu wa maisha ukizingatia alihitaji Malazi, huduma za afya na malezi ya karibu sana. Ally alihangaika  huku na kule na kujikuta anaishia mitaani na kuwa ombaomba.

Katika safari yake alifanikiwa pia kufika Hospitali ya KCMC Moshi walikomtibu kwa muda mfupi na kumhakikishia kuwa kama atamudu gharama za hapo wanaweza kumuwekewa mikono bandia itayomuwezesha kufanya  shughuli ndogodogo zinazoweza kumuingizia kipato bila kutegemea watu.
Kutokana na hali duni ya maisha Ally aliamua kuingia mtaani tena na kuanza  kuomba kutoka kwa watu mbalimbali, ila safari hii akiwa na nia ya kutimiza  ndoto ya kupata hela itayomuwezesha kununulia mikono mipya ya bandia. Maisha ya kuombaomba  hayakuwa rahisi kwa Ally na hivyo kuishia kupata hela ya kula na matibabu ya vidonda alivyonavyo. Kwa kuona hili KCMC waliamua kumuandikia barua itayomjulisha mtu yoyote nini Ally anahitaji kutoka kwao
Katika tatizo hili Ally alijaribu pia kupitia sehemu mbalimbali ikiwemo ofisi za Serikali, Taasisi, Wafanyabiashara na vyombo mbalimbali ikiwemo baadhi ya Luninga  bila mafanikio hadi sasa. Ally bado ana ndoto ya kubadili maisha yake iwapo atabahatika kupata mikono hiyo, Ally bado anaendelea kuomba  kwa kutumia  msaada wa barua aliyoandikiwa na Serikali ya Mtaa huko Mbagala - Makuka ila hela hiyo anayopata  imekuwa ikitumika kwa matumizi yake ya kila na familia yake bila kukidhi gharama za hospitali na wala hazitoshi  kununua mikono bandia.

Gharama za Matibabu ya Ally kwa sasa

1.      Gharama za mikono (Angalia invoice hii hapa juu)
Tshs . 4,000,000

2.      Nauli ya kwenda na kurudi Moshi kwa watu wawili
Ally na Mkewe na kula njiani
60,000 x 2 = 120,000

3.        Gharama za Makazi kwa siku 31
15,000 x 31 = 465,000

4.       Gharama za Chakula kwa siku 31
10,000 x 31 = 310,000

5.      Gharama ya Usafiri wa daladala akiwa Moshi kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa siku 31
1,200 x 31 = 37,000

Jumla ya gharama yote ni Tsh. 4,587,000


Kama itapatikana Tshs. 5,000,000 itatimiza lengo kufanikiwa kubakiwa na 413,000 itayomuwezesha Ally kuanzisha biashara ya genge.

inahitajika  marafiki   10,000 (Elfu kumi)  wataoweza kuchangia  Tshs. 500
 kila mmoja  10,000  x 500 = 5,000,000

·        Kwa kuchangia matibabu ya Ally Habibu Kieki tuma kuanzia shilling 500 kwenda kwa  Tigo pesa kwa No ya Ally Habib Kieki no 0719 - 593007

·        Kwa Maelezo zaidi kuhusu Kampeni hii piga simu Kwa Dada Jennifer 0712- 221744


·        Kwa kuwasiliana na Kaka Ally mwenyewe na kupata maelezo kuhusu afya yake piga simu 0714 - 080360


“ Shiling 500 yako inaweza kubadili maisha ya Ally – Shime wote”



No comments:

Post a Comment