Thursday, 24 January 2013

AIBU YA MKE WA MTU KUCHOJOA NGUO ZOTE KWA UTAMU WA BENDI!!!KITUKO cha aina yake kimejiri Jumamosi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar wakati Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilipokuwa ikitumbuiza, Amani linakumegea kilichotokea.
Katika onesho hilo, mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu alifanya kitendo cha aibu baada ya kusaula nguo zake zote na kubakia na nguo za ndani.
Katika onesho hilo, Extra Bongo ilikuwa ikiwashindanisha mashabiki wake kucheza staili yao ya Kizigo na washindi kujinyakulia zawadi za fedha.
Wakati bendi hiyo inayoongozwa na ‘Kamarade’ Ally Choki ikitoa burudani, ghafla mwanamke huyo (jina lake halikupatikana) alivamia jukwaa na kuanza kucheza kwa staili aliyokuwa akiijua mwenyewe.
Mpigapicha  alipojaribu kumpiga picha dada huyo alihamaki na kumjia juu huku kumtishia kumvunjia kamera yake huku akidai kuwa yeye ni mke wa mtu, hivyo hapaswi kupigwa picha.
“Mimi ni mke wa mtu ukifanya mchezo nitakutolea laana,” alisema mwanamke huyo huku akizishika nguo zake na kuanza kuzitoa mwilini mwake  moja baada ya nyingine.
Wakati mwanamke huyo akiendelea na zoezi lake la kusaula nguo, alijitokeza dada mwingine ambaye  aliambatana naye pamoja ukumbini hapo na kumwita  kwa jina la wifi.
“Wifiii…, wifiii…, weee wifii pombe gani hizo, usivue nguo, usifanye hivyo ni aibu,  itakuwaje kaka akiziona hizo picha magazetini?” alisema dada huyo aliyedaiwa kuwa ni wifi mtu lakini pamoja na kumpigia kelele hizo haikusaidia kumzuia  mwanamke huyo mcharuko kusaula nguo zake.
Baada ya kuombwa sana na wifi yake, mwanamke huyo alivaa nguo zake na kuendelea na burudani hadi mwisho.
Haikufahamika mara moja kama mwanamke huyo alifanya  kitendo hicho kutokana na pombe au hasira za kupigwa picha.
Chanzo:globalpublishers

No comments:

Post a Comment