Thursday, 4 April 2013
Abambwa akidaiwa kuuza mtoto mil.1/-
TABU Mwashipete (40) mkazi wa Kijiji cha Mpemba, wilayani Momba, Mkoa wa Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutaka kumuuza Hosea Mwashipete (5) mtoto wa kaka yake Simon Mwashipete.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Diwani Athumani alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa anamuuza mtoto huyo kwa sh 1,000,000 kwa mkazi wa Mpemba, John Sinyinza.
Alisema mama mzazi wa mtoto huyo alifariki dunia, hivyo alikuwa anaishi na shangazi yake.
Kwa mujibu wa kamanda, sababu za mtuhumiwa huyo kumuuza mtoto ni kupata fedha kwa ajili ya kumsaidia kaka yake katika kesi ya mauaji inayomkabili.
Alisema mnunuzi alitoa pesa za malipo ya awali ambazo walikubaliana atoe sh 100,000 ambapo alienda kutoa taarifa polisi hivyo polisi walifanya mtego na mtuhumiwa alikamatwa.
Hata hivyo alisema taratibu za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa zinafanywa ili iwe fundisho kwa wengine.
chanzo:daima
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment