Friday 26 April 2013

Ray: Siumwi jamani


MWIGIZAJI na muongozaji wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameamua kuvunja ukimya na kudai kwamba kupungua kwake mwili sio kwamba anaumwa bali ni katika kubadilisha muonekano wake.
Akifunguka katika kipindi cha ‘Action Cut’ kinachorushwa na Chanel Ten, Ray alisema kumekuwepo na maneno mengi yanasemwa na watu na mengine kumfikia kuwa kuna kitu kinamuuma, hivyo ni bora aombe msaada mapema ili aweze kusaidiwa.
“Jamani nataka kuwahakikishia mashabiki wangu kuwa sina panaponiuma bali nimeamua 
kuutengeneza tu mwili wangu kama wafanyavyo mastaa wa nje na kutokana na hali hii, sasa hivi naweza kucheza nafasi mbalimbali, ikiwemo kupigana, mwanafunzi na wategemee kuniona katika aina nyingine ya uigizaji na siyo ile waliyonizoea,” alibainisha Ray.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment