Monday 10 June 2013

Hadithi,Hadithi.......Hadithi njooooo utamu koleaaa... BINADAMU HANA WEMA toleo la 2

Mfalme akatoa zawadi kwamba mtu atakayempata binti yake atapata kuwa mfalme na yeye atakuwa chini yake.

Siku moja yule binadamu aliyeokolewa na Sande kule msituni akaamua kwenda kumtembelea Sande. Alipofika hapo akamkuta yule binti wa mfalme, akashtuka sana akajisemea moyoni mwake, "Hivi yule binti wa kifalme anayetafutwa si ndiyo huyu, nikitoka hapo naenda kupeleka taarifa kwa mfalme"

Sande asijue nini kinachoendelea huko kwenye nchi ya watu na wala asijue aliwazalo yule rafiki yake mnafiki, akafurahi sana kutembelewa na rafiki huyo na kumtambulisha mke wake bila kuhofu chochote.

yule binadamu akaongea ilipofika jioni akaaga akaondoka. Yule binadamu alipotoka pale nyumbani kwa Sande safari yake ikawa moja kwa moja mpaka nyumbani kwa mfalme na kutoa taarifa ya kumuona binti ya mfalme.

Mfalme akaamuru jeshi lake likaenda na yule binadamu mpaka kule msituni, wakamchukua Sande wakampeleka mpaka kwa mfalme. Na Mfalme akatoa adhabu ya kifo kwa Sande.
Lakini wakati wanasubiri saa ya hukumu hiyo kutekelezwa, Sande akiwa amefungiwa kwenye chumba cha mateso mara akatokea nyoka.

Akamwambia, "Rafiki, unakumbuka siku ile wakati unatuokoa kule shimoni tulikwambia nini? sasa umeamini mwenyewe yale maneno tuliyokwambia?"

Sande hakuwa na kujibu zaidi ya kulia tu. Nyoka akamwambia, "nitakusaidia rafiki usilie sana."
Nyoka akatoka, alivyorudi alikuwa ameshika majani, akamwambia

 "Unayaona haya majani, hii ni dawa ya nyoka, mimi nitaenda kumgonga mfalme nikitoka hapa, hakuna mganga yoyote atakayeweza kumponya mfalme ila ni wewe peke yako, sasa usisahau."
Sande akasema sawa, sasa na matumaini ya kuendelea kuishi tena yakarejea tena.

Nyoka akatoka pale akaenda moja kwa moja mpaka kwenye nyumba ya mfalme, akamfata mfalme akamgonga kisha akakimbia. Mfalme aliumwa sana, waliitwa waganga wote wa nchi ile kwa ajili ya kumtibu mfalme lakini walishindwa.

Hatimaye mmoja akatoa wazo la kuitwa kwa Sande kwani alisema inawezekana akajua dawa kwa sababu ameishi sana msituni, wengi walidharau wakisema wameshindwa waganga mabingwa hapa nchini, itakuwa yeye!

Lakini mfalme akaamuru aitwe Sande, Sande alipopata taarifa hiyo alifurahi sana akaenda zake polini akachukua yale majani aliyoambiwa na nyoka akenda akayaponda akamkamulia Mfalme, na mfalme akapona.

Mfalme akatangaza kuanzia siku ile Sande ndiye mfalme wa nchi ile na yeye mfalme atakuwa chini yake na akamkabidhi Sande yule binti ili awe mke wake. 

NA HADITHI YANGU IMEISHIA HAPO

MLIO KOSA TOLEO LA NO 1

No comments:

Post a Comment