Imamu wa msikiti wa Maziwa Ngo’mbe Kisiwani Pemba, Omar Hussen Said (42), amepigwa na kujeruhiwa jicho baada ya kutokea vurugu ndani ya msikiti wakati wa ibada ya Ijumaa iliyopita.
Vurugu hizo zimesababishwa na baadhi ya waumini wa msikiti huo ambao wanapinga Imamu Said kuendelea kushika wadhifa huo kutokana na kitendo chake cha kujivua uanachama wa CUF na kujiunga na Chama tawala CCM mwaka huu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mohammed Shakani, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kwamba watu watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na shambulio dhidi ya kiongozi huyo wa dini.
Aliwataka watuhumiwa hao kuwa ni Mfaki Aambao ni wakazi wa Maziwa Ngo’mbe Wilaya ya Micheweni.
Shakani, alisema Jeshi la Polisi linamsaka Mbwana Haji Mbwana ambaye ametoroka kwa kukimbilia Unguja badaa ya tukio hilo.
“Watuhumiwa watafukishwa Mahakamani Jumatatu (leo) wakati Jeshi la Polisi tukiendelea kumsaka Mbwana Haji Mbwana ambaye ametorokea Unguja,” alisema Shakani.
Alisema wakati Imamu Said akitoa mawadha ya Ijumaa katika membari ya msikiti, alivamiwa na kuanza kupigwa na kujeruhiwa jicho la kushoto na kutibiwa katika Hospitali ya Micheweni.
Hata hivyo, alisema vurugu hizo zilidhibitiwa haraka kwa kutumia mtandao wa askari kazu waliokuwa wameimarisha ulinzi katika misikiti mbali mbali wakati wa ibada ya Ijumaa.
Alisema watu wanao tuhumiwa kuhusika na vurugu hizo wamekamatwa na kufunguliwa mashitaka katika kituo cha Polisi Micheweni. Alisema Imamu Said anaendelea vizuri baada ya kupata tiba.
Imamu Said ni kati ya wanachama 30 wa Chama cha wananchi CUF waliamua kukiama CUF na kujiunga na CCM na walipokelewa Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein Mei mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Ugunja, Dadi Faki Dadi, amewataka wananchi Mkoa humo kujiepusha na vitendo vya vurugu ikiwemo kuchukua sheria mkononi.
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment