Friday, 17 January 2014

Askofu anusurika jela

ASKOFU wa Kanisa la Habari Njema mjini hapa, Tryphone John, amenusurika kwenda jela baada ya  kulipa faini ya sh 30,000 baada ya kupatikana na hatia ya gari lake kumgonga mwendesha pikipiki, Mandikilo Baluhya (42) na kumsababishia ulemavu wa kudumu.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Geita baada ya kumtia hatiani na kumtaka kulipa faini hiyo ama kwenda jela miezi sita.
Awali akisoma maelezo ya kesi hiyo, Mwendesha Mashitaka, Janet Kisibo, alidai Aprili 29, mwaka jana akiwa mjini eneo la Shell ya Gedeco, Baluhya aliyekuwa akiendesha pikipiki T 272 BQT aligongwa na gari T 448 AGY  Toyota Hilux lililokuwa likiendeshwa na dereva George John ambaye ni mfanyakazi wa askofu huyo ambaye  alikimbia  baada ya ajali hiyo na mpaka sasa anaendelea kutafutwa.
Mwendesha mashitaka alidai tuhuma zilizomfikisha mahakamani askofu huyo ni kutotunza kumbukumbu za mtumishi wake.
Baluhya ambaye ni mkazi wa Mkolani mjini hapa, ambaye sasa amekatwa mguu kutokana na ajali hiyo,  alisema amekuwa akihitaji msaada wa kumuuguza tangu alipokuwa Hospitali ya Bugando, lakini askofu huyo hakumsikiliza zaidi ya kumpatia sh 300,000, kiasi ambacho hakikidhi mahitaji ya matibabu na kuhudumia familia. Alisema ana familia na mke mmoja na watoto tisa wanaomtegemea.
“Nikimpigia simu anakuwa mkali hataki kunisikiliza, anasema niende popote pale yeye ameshamaliza nisimsumbue,” alisema Mandikilo kwa uchungu huku akiomba wasamaria wema wamsaidie walichonacho ili anusuru afya yake na familia
chanzo: Tz daima

No comments:

Post a Comment