Thursday, 16 January 2014

Mtoto Elifrida achomwa moto wa nailoni na godoro




Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Julai 10, mwaka jana ambapo Elifrida aliyechukuliwa kutoka Kigoma kwa wazazi wake na kwenda kuishi Mkolani jijini hapa kwa shangazi yake, alijikuta akiambulia mateso makubwa yalimsababishia kupoteza vidole vyake vya mkono wa kulia kwa kuchomwa moto.
Akielezea jinsi ilivyokuwa, Elifrida ambaye kwa sasa analelewa katika kituo cha watoto waliofanyiwa ukatili cha Foundation alisema kwa uchungu:
“Nakumbuka siku hiyo shangazi alinifunga mikono na miguu kwa kamba na kuuzungushia mkono wake kipande cha godoro na kunifunga kwa ‘nailoni’ kisha akaniwasha moto mpaka moto ulipoisha, alinichia baada ya mimi kupiga makelele ya maumivu.


Shangazi yake huyo alifikishwa kituo cha polisi cha Igogo, Nyamagana na kupewa fomu ya PF-3 ambapo alipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Sengerema kwenye kitengo cha watu walioungua na moto kisha akapatiwa matibabu ambapo alilazimika kukatwa vidole vyake vilivyoathirika vibaya huku vingine vikiongezewa nyama aliyokatwa kutoka mapajani.
Akizungumza na waandishi wetu, mama wa Elifrida aliyejitambulisha kwa jina la Malina Fabian alisema anaomba msaada wa kisheria kwa kuwa kesi ya mtoto wake inachukua muda mrefu.
‘’Naomba jamani taasisi inayohusika na sheria ishughulikie kesi ya mtoto wangu kuharakisha maana ni muda mrefu sasa,’’ alisema mama wa mtoto huyo.
Awali, kesi ya mtoto huyo ilitakiwa kutajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mwishoni mwa mwaka jana lakini ilisemekana haikutajwa kutokana na sababu zisizofahamika ndipo tume ya haki za binadamu ilipoingilia kati kwa ajili ya kusikilizwa upya mahakamani hapo.
chanzo:.globalpublishers


No comments:

Post a Comment