Friday, 21 November 2014

Betty ameuawa kwa kupigwa risasi leo

DADA aliyefahamika kwa jina moja la Betty ameuawa kwa kupigwa risasi leo saa mbili asubuhi maeneo ya Yombo-Vituka, Temeke jijini Dar es Salaam akiwa kwenye gari aina ya Toyota Pick Up mali ya Tunu Security.
Marehemu Betty ameuawa na watu waliokuwa kwenye bodaboda wakati akiwa kwenye gari la Tunu Security akitokea kituo cha mafuta kuelekea benki.
Watu hao waliokuwa kwenye bodaboda mmoja alimpiga dereva wa gari risasi ya mkononi alafu akampiga Betty risasi ya kichwani huku mlinzi aliyekuwa katika gari hilo akikimbia ambapo watu hao walichukua mfuko uliokuwa na pesa na kutokomea kusikojulikana.
Baadaye mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi na kupelekwa Hospitali ya Chang'ombe,Dar kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
chanzo:GPL)

No comments:

Post a Comment