Msaada unahitajika kwa kijana Suleiman Othman Ally mwenye umri wa miaka 19, mkaazi wa Zanzibar, amepatwa na tatizo la uvimbe mkubwa kwenye mgongo wake baada ya kupatwa na ajali kugongwa na Vespa kwa muda wa siku nyingi tu, walimpeleka Hospitali ya Mnazi mmoja ambapo ilishindikana kupata matibabu kutokana na damu nyingi aliotoka wakati wa upasuaji, hivyo kuwalazimu kumshona bila ya kumfanyia operation iliyokuwa wamemkusudia.
Kijana Suleiman Othuman hali yake inazidi kudhoofika na maumivu makali alionayo kwa sasa hawezi kukaa kusimama vizuri na hata kulala inavyostahiki kwa sababu ya ule uvimbe aliokuwa nao kwenye kiuno chake kam picha inavyojionyesha.
Hivi sasa familia yake haina budi kuomba ushirikiano wa msaada wenu kwa ajili ya kuweza kumpeleka nchini India kwaajili ya matibabu na kumgharamikia mtu wa kufuatana nae katika familia, kutokana na gharama ni kubwa na uwezo ni mdogo.
Hivi sasa yuko hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12.
Ndugu zangu tujitahidini kuokoa maisha ya ndugu yetu Suleiman Othuman kwa hali na mali.
Kwa mtu yoyote atakayeguswa na habari hii, na mwenye kutaka kuchangia msaada wake anaweza kuwasiliana na Mama yake mkubwa. Bi Salma.
Numba yaze za simu ni-:
255777489015
Tigo: 255655489015
chanzo:http://swahilivilla.blogspot
No comments:
Post a Comment