Friday 21 November 2014

Papa Msofe kuendelea kusota lupango


MFANYABIASHARA anayekabiliwa na kesi ya mauaji, Marijan Abubakar, maarufu kama Papa Msofe na mwenzake, Makongoro Joseph, wameendelea kusota rumande kutokana na kile kinachoelezwa ni upelelezi kusubiriwa ukamilike.
Kesi ya watuhumiwa hao wawili ilitajwa jana na Mwendesha mashitaka wa serikali, Adolph Mkini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi, Franki Moshi.
Hata hvyo, Hakimu Moshi aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 25, mwaka huu itakapotajwa tena. Makongoro na Musofe wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kitoli wanalodaiwa kulitenda mnamo Oktoba 11, 2011.
Wakati huo huo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeipiga kalenda kesi ya washitakiwa 10 wa mauji ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Edmund Mvungi kutokana na upelelezi kutokamilika.
Kesi hiyo ilihairishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Mbando mpaka Desemba 2, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa. Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Chibago Magozi (32), Longishu Losingo (29), Masunga Makenza (40), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Zacharia Msese (33), Msungwa Matonya (30) na Ahmad Kitabu (30).
Kwa pamoja wanadaiwa kuwa mnamo Novemba 3, mwaka 2013, walifanya kosa hilo la mauaji ya kukusudia kinyume na kifungu cha 196 cha sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
chanzo:tzdaima

No comments:

Post a Comment